TUNGO ZA KUJIBIZANA: "KUAMBIZANA NI SIFA YA KUPENDANA"t



Similar documents
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA BILL SUPPLEMENT

THE OIL AND GAS REVENUES MANAGEMENT ACT, 2015 ARRANGEMENT OF SECTIONS PART I PRELIMINARY PROVISIONS PART II ADMINISTRATIVE PROVISIONS

Linking Adult Education with Formal Schooling in Tanzania: Mission Unfulfilled

Lesson 14a: Numbers and Counting

TANZANIA COFFEE BOARD VACANCIES ANNOUNCEMENT

Contents Page. 3. Financial Highlights 4-8. Chairman s Statement CEO s Statement

Annual Report and Financial Statements

EXISTENTIALISM AND FEMINISM IN KEZILAHABI S NOVEL KICHWAMAJI

MARX'S SHORTS AND ANCESTORS' CAVES: TRACING CRITICAL MOTIFS IN KEZILAHABI'S PLAY AND POEMS*

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Januari, 2015

Contents. CORE VALUES Integrity Professionalism Team Spirit Safety Culture. Company Information 2 Message from the Chairman 4

Lesson 56: Business: [biashara: ununuzi, upigaji bei na uuzaji] Business: Shopping, Buying and Selling. A). Business Vocabulary.

OPERATIONS MANUAL FOR IMPLEMENTATION AND MANAGEMENT OF A COMMUNITY HEALTH FUND in Tanga Region

Annual Report Report and and Financial Statements

Creation of a Speech to Text System for Kiswahili

DAR ES SALAAM UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION. A Constituent College of the University of Dar Es Salaam STAFF FUNERAL POLICY

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION CKRC VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, SABOTI CONSTITUENCY, HELD AT KITALE TOWN MUSEUM HALL

ROMAN CATHOLIC FAITH REPRESENTED IN KEZILAHABI'S MZINGILE SONJA MEZGER AAP 72 (2002) SWAHILI FORUM IX 75-85

THE ANTI-MONEY LAUNDERING ACT,2006

KUKITANDAWAZISHA KISWAHILI KUPITIA SIMU ZA KIGANJANI: TAFAKARI KUHUSU ISIMUJAMII

TANZANIA AND HIV/AIDS TANZANIA NA UKIMWI

Centum Investment Company Limited Annual Report & Financial Statements fy 13/14

Uundaji wa Istilahi za Kiswahili Kileksikografia na Athari zake S.S. SEWANGI University of Dar-es-Salaam, Tanzania

MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

DR. HAMISI O. BABUSA (PHD)

TEGENI MASIKIO: COMPOSING EAST AFRICAN REALITIES THROUGH YOUNG EYES

A SHABA SWAHILI LIFE HISTORY: TEXT AND TRANSLATION

Je! Mungu Habadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

Ndugu na dada zangu. Mbio za Maisha

KANISA LINAHITAJI KUJUA

LUGHA YA MITAANI IN TANZANIA THE POETICS AND SOCIOLOGY OF A YOUNG URBAN STYLE OF SPEAKING

Yaliyomo. II. Dodoso la Kilimo... 62

Mwalimu Nyerere Engages His People: Scripture Translation in Swahili Verse

Celebration of the French «Bastille Day» Remarks by Ambassador Elisabeth Barbier 14th July 2010

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,

LEARNING HOW TO TEACH

Ni Wakati Wa Kuamka! Ellis P. Forsman. Ni Wakati Wa Kuamka (It's Time To Wake Up) 1

CURRICULUM INNOVATION IN TEACHER EDUCATION

Kitabu hiki kimefanikishwa kwa msaada wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates

KISWAHILI Pam Inoti - pamby22@gmail.com

MORE SWAHILI PROVERBS FROM EAST AFRICA METHALI ZAIDI ZA KISWAHILI TOKA AFRIKA MASHARIKI. L. Kalugila. A. Y. Lodhi

CONTENTS. Financial Section. Sehemu ya Kiswahili. Statutory Information

Tunza Jamii Yako, Tunza Mazingira Yako kwa Maisha Bora. Jihusishe. Jipangie. Amua

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF

815 SWA. Health undertaking Kuwajibika Kiafya. Tafadhali weka kurasa hii ya maelezo kama kumbukumbu yako

Sda Church Nyimbo Za Kristo

TRAINING ON ENTREPRENEURSHIP AND BUSINESS MANAGEMENT SKILLS FOR SELECTED VILLAGERS IN RUFIJI

Lesson 24: Adjectives

ANNUAL REPORT 2015 THE TASKS OF TBL INTRODUCING

Teach Yourself Swahili

Tuko Pamoja. Adolescent Reproductive Health and Life Skills Curriculum

Language Choice in Swahili Newspaper Advertising in Tanzania

Lourenco Noronha. Lektor ( für Swahili Literatur am Institut für Afrikawissenschaften der Universität Wien

HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII MKOA WA DODOMA

ACADRI 2015 TRAINING PROGRAMMES

MWONGOZO WA USHIRIKISHWAJI KATIKA KUPANGA MATUMIZI YA ARDHI WORLD BANK

TAARIFA YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA UKIMWI MKOA WA KIGOMA

Aga Khan University College Tanzania. Catholic University of Health and AlliedSciences (Bugando) Dar es Salaam Institute of Technology

CUF. Rais makini, Serikali makini Uchumi Imara, Mabadiliko Sahihi

Promoting Regional Trade to Enhance Food Security

Ambassador s Community Grants Fund for HIV/AIDS Relief

Vidunda (G38) as an Endangered Language?

Mother Tongue Theological Education in Africa: A Response to Jim Harries The Prospects for Mother Tongue Theological Education in Western Kenya

The mother, her confidants and the prevention of mother-to-child transmission of HIV (PMTCT) services in the Kilimanjaro region, Tanzania

CURRICULUM VITAE PERSONAL DETAILS. Prof. Wanyama Mellitus Nyongesa. Age: 47. Associate Professor of Musicology at Moi University, Eldoret, Kenya

MEANING AS USE: A FUNCTIONAL VIEW OF SEMANTICS AND PRAGMATICS

CURRICULUM VITAE. 1. SUMMARY OF EXPERIENCE Special Needs Education Lecturer Psycho-educational Assessment Professional

The linguistic situation in Tanzania

Girls Getting to Secondary School Safely: Combating Gender-based Violence in the Transportation Sector in Tanzania

Swahili. Information provided by: National African Language Resource Center (NALRC)

Having ready access to contraception entails an

Towards Full Comprehension of Swahili Natural Language Statements for Database Querying

ARMS CONTROL Volume 3 Issue 1 May 2011

OLD BUILDINGS RESTORATION TECHNIQUE. Dr-Ing JK Makunza University of Dar es Salaam 18 th May 2011

The Mosaic Project Theme Song 2001 The Mosaic Project Music by Brett Dennen, Lyrics by Brett Dennen and Lara Mendel

CURRICULUM VITAE Tutorial Fellow, Department of Theatre Arts and Film Technology, Kenyatta University

TANZANIA PARALEGAL BASELINE SURVEY

2009 Ph.D., Applied Linguistics with an emphasis on Discourse Analysis and Sociolinguistics, University of Illinois at Urbana-Champaign.

Winners, cheats and witches: East African soccer cartoons Beez, Jigal

D36. Core Analysis Frame: Poetry. Examine Content. Examine Form and Structure. (continued on page D37)


The United Republic of Tanzania


1. TASAF operations steadily approaching set targets

MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING

TEKNOLOJIA ZA UTAYARISHAJI, USINDIKAJI NA HIFADHI YA MAZAO YA MBEGU ZA MAFUTA BAADA YA KUVUNA. Kitabu Namba 5

L E A P n e w s. Tahariri. Editor s note. Number 15/16 September December 2007 Newsletter of the Language in Education in Africa Project

DECLARATION OF PERFORMANCE NO. HU-DOP_TN _001

UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

Headline News Analysis. Top-Ranking Headline Stories

NEGOTIATING THE NEW TUKI ENGLISH-SW AHILI DICTIONARY A CRITIQUE FROM A PEDAGOGICAL AND SCHOLARLY PERSPECTIVE'


1.- L a m e j o r o p c ió n e s c l o na r e l d i s co ( s e e x p li c a r á d es p u é s ).

Lesson 43: Commands. D). Commands may take object markers to indicate the recipient of a command

Tense and aspect in Swahili

Section 2 Assessment

Integrated Logistics System (ILS) Procedures Manual

The Story of Swahili

Literacy Overview - Sheringdale Year 1

1. imagery 2. plot 3. foreshadowing. 10. structure 11. symbol 12. narrative. 13. motif 14. conflict 15. theme

Transcription:

AAP 47 (1996) 1-10 TUNGO ZA KUJIBIZANA: "KUAMBIZANA NI SIFA YA KUPENDANA"t RIDDER SAMSOM Different labels have been used for marking the reciprocity in Swahili dialogue poetry, varying between the more neutral 'malumbano' or 'kujibizana' and the more marked 'ukinzani' or 'mashindano' By showing a satnple fiom the Zanzibari newspaper Mwongozi (1956) of a poetic dialogue on wife-husband relationships, the paper argues that the poetical form and the strong language used ate not a mere expression of what has been called 'rivalry', but instruments in expressing views and opinions that have been observed in other literary devices (mithali, misemo, vijembe) and their usage At the same time it is demonstrated that different types of poems (tenzi, mashairi, nyimbo) and different styles (plain, metaphoric, riddle) are used side by side The atnbiguity, incompleteness and strength of the language that is used in this poetry, make it all possible to express views on sensitive issues in the society Maneno ya sentensi hii 'kuambizana ni sifa ya kupendana' yangeweza kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye kanga ( au watn wengine huiita leso ), bali ni jina la utenzi mfupi uliokuwa wa sita katika mfululizo wa tenzi kama kumi hivi. Hizo zimetoka katika gazeti la Mwongo'Tl hnko Zanzibar ku~n-na tarehe 25 Mei 1956 na kuendelea haill mwe'71 wa kumi na moja wa mwaka ule ule.. I enzi zote hizi zilihusu swala la uhusiano baina ya wake na waume zao Zilikuwa zimetungwa na wanawake na wanaume pia Kabla sijaanza kuchambua hizo tenzi zenyewe, nataka kwanza nionyeshe 'kuambizana' huku kuna maana gani katika jamii na fasihi ya Kiswahili, kwani 'kuambizana' ni 'kupeana shauri', yaani kuambiana kwenye madhumuni maalum Ufasaha wa lugha ni jambo muhinm katika ustaarabu wa Kiswahili Wasomi wengi waliochambua na kutafiti jamii hii husisitiza umuhimu huu wa kuweza kutnmia lugha isiwe chombo cha mawasilano tn, bali itnmike kwa ustadi na ubingwa. Mtn mwenye ufasaha na usanifu wa lugha huheshlmwa na si mhisi kupewa hadhi au cheo hila kuwa na ustadi wa lugha U stadi huo si wa kutunga au kubuni tn, bali pia ni ustadi wa kutnmia lugha fasaha kila panapohitajika Matnmizi ya lugha fasaha inayofaa muktadha (yaani 'context') fulani yamesababisha kuwepo funi mbalimbali za fusibi au, tnseme, ustaarabu au utamaduni wa lugha, kama vile mithali, vitandawili, vijembe, nyimbo, matumizi ya lugha kwenye kanga, na aina za ushairi. Fani hizo nilizotaja, ingawa zinatofautiana kifasihi, zinalingana katika jambo moja: hutnmiwa na wasemaji katika hali ya aina ya mashindano Maana, kwa kutumia mithali mtn hutaka kusisitiza msintamo wake kwa usemi mfupi unaokubalika na jamii yote; kwa kitandawili kuna mashindano ya 'kufunga na kufungua mnyama'; vijembe vinawakata wazungumzaji kama kisu; nyimbo, hasa nyimbo za taarab au nyimbo za hamsi, mara nyingi 1 Shukrani zangu ziwaendee Hatnad B Mshindo (Zanzibar) na Sauda A I Barwani (Hatnburg) kwa ushauri wao kuhusu matumizi ya lugha

2 RIDDER SAMSOM husikika katika hali ya mashindano fulani; kanga zenye misemo yake huenda ni jawabu fulani katika hali watu wanayoshindania. Aina moja ya ushaiii hujulikana kama 'malumbano', pengine huitwa 'kujibizana', kwa Kiingereza wasomi wengi hutumia 'dialogue verse'. Hadi sasa viineandikwa vitabu viwili kuhusu ushaiii huo wa kt!iibizana. Kimoja ni kitabu cha lbralllin Noor Shaiif ambacho kilikuwa sha!iada yake ya uzamili (PhD) 'The Function of Dialogue Poetry m Swa!Iili Society' (1983) Cha pili ambacho mwandishi wake ni Assibi A Amidu killahusu ama maalum ya ushaiii wa kujibizana huko Lamu mayoitwa 'Kimwondo' (1990}. Naye Shaaban Robert katika 'Maisha Y angu na Baada ya Miaka Hamsilli' aliandika msha 'Ukinzani' ambayo ndani yake alitaja baadhi ya mashaiii yaliyotokea gazetilli yakitetea shaiii lake 'Ujane'. Madhumuni ya makala hii ni kutoa mfano wa ushaiii wa kl.!iibizana na kutazama hayo mashindano ambayo yameitwa 'rivahy' na Hanies (1966) na wengine, yana maana gani na iwapo kweli ni mashindano au la. Sasa tutazame tungo zenyewe.. Wa kwanza ulitokea katika gazeti la Mwongozi la tarehe 25 Mei 25 1956 (taz NYONGEZA mwishoni mwa makala hii). Utenzi mfupi huu una beti 20 na kutiwa sailli kwa jma la AI-Mukhlisa. Hilojma nijma la ushaiii aujma la kujificha nalo, maana yake matokana na neno la Kiarabu 'mukhlis', yaani mwaminifu, mtu mwenye moyo safi na msema kweli pia. Kwa sababu ya mnyambuliko wa mwisho wa jma hilo Al-Mukhlisa, tunajua mtu huyu ni mwanamke, na haya yamethibitishwa pia na jma la utenzi wenyewe, kwani juu yake imeandikwa 'Wanawake Tufanyeje?' Maudhui ('content') yake, yaani kiiiii cha ujumbe wake umeelezwa wazi kabisa katika ubeti kwa kwanza ambao ni: (1) Bismzllahi awalz Waume wenye akili nanena yangu kauli wameihama dunia Halafu mshaiii anaeleza kwa nini anawaona waume wametokwa na akili: hawashughulikii wake zao, hawajali ndoa, hawawapi wanayohitaji kwa malezi ya watoto, mavazi, na pesa W akati wa Ramadhani ni wakali na kutofuata sharia za kutoa zaka: ( 4) Nyumba wanazzpuuza Hawawezi kutimiza wake wanawachagiza ahadi walizotoa Kwa upande wa wake haiwasaidii kulalamika Wanawake wakisema au wakillyamaza mambo ni yale yale, hutolewa ukali tu, hukiinbiwa nyumbani kwao, waume 'hugeuka vzpepeo, kuruka wakakimbia' Na ikiwa wanawake wanalalamika mno, ~m moja hupewa talaka na hata baadaye kutopata haki zao pamoja na watoto: (16) Mtoto hutoka ;asho Njoo Ieo njoo kesho akenda kutaka posho huzungushwa kama pia Kwa jumla mshaiii anasema kwamba hayasemeki kwa kiasi gani wanawake walivyo na dhiki na kujuta kuolewa Mshaiii anajiuliza maswali mawili. La kwanza ni jma lenyewe la utenzi, 'Wanawake tufanyeje?', na linajibika katika mwisho wa utenzi: tujiombee Mungu atusaidie na tu we na subiia. Swali la pili analojiuliza mshaiii ni kwa nini hao waume huwatendea wake zao

IUNGO ZA KUJIBIZANA 3 hivyo Rapa ndipo katika utenzi anapowasemesha wanaume na mwenyewe kukataa kujibu swalihilo: (7) Lipi linawakimbiza Wake wanawaliwaza waume we tu nawaza nyumbani mkzingia Lugha anayotumia si ngumu wala yenye tashbiha ('simile') na sitiari ('metaphor') nyingi au mafumbo ambayo yanahitaji werevu mkubwa wa kuyafumbua. Rata hivyo mara nyengine anatumia picha fulani kuelezea tabia ya mtu, kwa mfano anawaita wanaume 'vipepeo', au misemo kadhaa kama vile 'kuihama dunia', 'kuwatupa mbali', 'hawajali wala hawabali', 'kutoka jasho' na 'kwenda akhera' Msamiati si mgumu pia, huenda anatia maneno yenye asili ya Kiarabu, km. 'nikaha' kwa ndoa au 'kuwadia' kwa kufika, lakini maneno kama hayo ni maneno ya msamiati wa msingi wa Kiswahili kinachosemwa Zanzibar Mara moja tu anabuni neno jipya ambalo maana yake inaeleweka kutokana na msingi, muktadha na vina vyake: ubabazi, yaani ubabaifu. Rata hivyo neno hili linaweza kuwa limekosewa tu katika uchapishaji, kwani neno 'ubabazi' lingefaa kabisa katika muktadha huu: ( 11) Kifika mwiyho wa mwezi hujztia ubabazi Waume hawmikizi lo lote utawambia Ingawa tungo nyingi zilizotoka katika gazeti ni za aina ya shaiii, utungo huu ulitungwa katika umbo la utenzi: yaani ubeti =oja una mishormo miwili yenye mizani 16.. Mishmoro hiyo ina vina vitatu, kati na mwisho wa mshomm wa kwanza na kati ya mshomro wa pili Kila irabu ya m-i7:1n-i ya mwi,..ho wa ubeti ina v...nia katika beti zote. Kila m_~hoioro nna mlzani 16 Uchambuzi na istilahi hizi zinatokana na Ibrahim Nom Sharif (1958:51) Kaluta Atmi Abedi huchambua utungo wa utenzi kwa nanma nyengine: 'ni ushaiii wenye mizani chache kuliko 12, ambao mata nyingi hauna vina vya kati katika mistari, bali kila ubeti una vina vya nanma moja katika mistari yake isipokuwa mstari wa mwisho katika kila ubeti, ambao huendelea na kina cha nanma moja kinachoitwa bahari. I enzi nyingi zaidi huwa zenye mistari mine na mizani minane' (1954:29) Tenzi tunazozungumzia hapa zinafuata uchambuzi wa Kaluta Atmi Abedi kwa vile ziinechapishwa gazetini zenye mistmi mine Bila shaka uchambuzi wa Ibrahim Nom Sharif unatokana na amdhi ('prosody') ya tenzi zinapoiinbwa. Uchambuzi wake unahusiana na sauti za tungo, sauti za ngoma na mahadhi ('melody') yake.. Inavyoonekana tofauti kati ya wasomi hao wawili inatokana na tofauti kati ya fasihi inayoandikwa na kusomeka tu na fasihi inayoiinbwa na kusikika Basi, suala hilo haliwezi kutatuliwa hapa kwani vipi tujue nini inatokea kichwani au moyoni mwa msomaji au mtungaji anaposoma au kutunga utungo fulani: husoma tu au anasikia na kuiinba vile vile? Utenzi huu 'Wanawake tujanyeje' ulitaka jawabu na kweli jawabu zilikuwa zikiingia ofisini kwa wahariii wa gazeti la Mwongozi Baada ya wiki tatu, yaani tarehe 15 Juni, tenzi mbili zilichapishwa kwenye ukurasa wa sita.. Mmoja ulitungwa na mwana=e kutoka Pemba aitwaye Salum Muha=ed Khamis Sheibany, mwengine na mwanamke aliyeitwa Moza Ali kutoka Zanzibar Utenzi wa kwanza unaitwa 'Bora MsingaliYema' na una beti 17 Msintamo wa mshaiii Salum Muha=ed unadhihirika mara katika mwanzo wa utenzi wake. Baada ya ubeti wa kwanza:

4 RIDDER SAMSOM (1) Naanza Bismi-lahi Kulcujibu nitawahi natunga nikifurahi Bintil-Mukhlisa anaendelea: (2) Hayo uliyoyanena si makosa ya mabwana Bali nanyi kina mama upenzini kujitoa Anaeleza kwamba si kwa sababu ya waume ndoa kuhmibika, bali wanawake, wao ndio chanzo cha balaa zote. Wana majivuno, wanawajibu waume zao kwa ~jemi, wenyewe wamejitoa upenzini Wanaume h~jitahidi ndoa kufanikiwa, huchapa kazi kupata rizki yao, wengine wanabaki maskini ingawa wako njiani tu wapate chochote Lakini hizo jitihada zote za bme tu, kwani: (9) Unaporudi nyumbani Bibi yupo mlangoni kuitia kitu tumboni wima kokusimamia (10) Hapo utamnasihi Ni nini cha ikrahi kumuuliza asahi kwako kilo kutokea Hatimaye mshairi anaishia utenzi wake kwa kuwaombea wanawake dua na kuwapa mawaidha: ( 17) Tiyalie kupendana Wazee na wao wana kwa mabibi na mabwana Isilamu wote pia Katika kumjibu Al-Mukhlisa mshairi anatumia dhana nyingi zilizokuwa zimetumika katika utenzi anaojibu: haja ya kutimiza alradi, kukumbuka shmia, kuwepo njiani, kuwepo kwa balaa, kuzingatia fikra. Analinganisha shida kati ya mke na mume na ndwele, neno la Kipemba na Kimvita ambalo maana yake ni IDaiadhi Lakini kama Mukhlisa mwenyewe, Salum Muhammed pia hajui sababu ya hayo yote, ila tu kujitoa kwa wanawake upenzini: ( 11) Hutatambua asili Kukujibu kwa fedhuli tadhani ni radi kali mwisho utajichukia Jawabu la pili ni utenzi wenye beti 10 wa Moza Ali Huyo alikuwa ni mshairi aliyfjulikana sana huko Zanzibar wakati wa harakati za kupigania uhmu Kati ya mwaka 1952 na 1964 zaidi ya tungo zake 80 zilikuwa zimechapishwa katika gazeti la Mwongozi. Jan Knappert alichapisha utenzi wake wa abjadi 'Adhabu za Jalrannamu' katika jarida la "Swalrili Journal" (1964} Nao akina Sengo wamewahi kuhariri mashairi yake machache katika 'Mashairi ya Mfungo wa Ramadhani' (1979}. Sauda Sheikh na Eleonore Adwiraalr walitoa mashairi matatu na habari za maisha yake katika 'Moza Ali, eine Dichterin aus Zanzibar' ( 1983) Anretajwa pia katika 'History of Kiswalrili Poetry [AD 1000-2000]' waliyofanya ISYSengo na M.M Mulokozi (1995) Washairi 29 wa Pemba na Unguja walipoulizwa nao, ni nani mshairi mwanamke ambaye kazi yake wanaipenda hasa, walikuwa wakinrweka Siti binti Saad awe wa kwanza naye Moza Ali wa pili (Uk 84) Wakati alipotunga utenzi huu mfupi ulio na beti kumi tu, alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja Aliuita 'Mukhlisa nakuwasa' Lakini hamwonyi Mukhlisa tu na kumwambza 'kwanz umekasa sana kuwatukana mabwana', bali anawataja watu wengine watatu. Mmoja wao

TUNGO ZA KUJIBIZANA 5 anamtolea mwito kuwanyamazisha wengine; wawili wengine anawalanmu kwa kuingilia kwa 'ukali' na kwa 'vigudi' na 'makeke makeke' Inavyoelekea, gazetini zilikuwemo tungo zao kati ya utenzi wa Mukhlisa na hizo mbili za Salnm Muhammed na Moza Ali Mwongozi ilikuwa ni gazeti la kila wiki. Kwa bahati mbaya matoleo mawili ya tarehe Mosi Juni na 8 Juni hayakupatikana katika Nyaraka za Zanzibar wala Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 2 Rata hivyo ni dhahiti kwamba wanaume wawili wameshajibu utenzi wa Mukhlisa na, kufuatana na Moza Ali, kutunga tenzi zao zenye hamaki na ukali: (7) Khasa Shekhe Aswedi Kutujiya kwa vigudi hamaki zimemzidi na kutukana vibaya (9) Naye Bwana El Mauli Jama hayo si halali mara katawa ukali ya dhma kushangiliya Ujnmbe wa mshairi huyu una vipengele viwili Kwanza anamwambia Mukhlisa ikiwa mwanamme mmoja anakosa, sio wote walio wabaya: (3) Kama kakosa mmoja siryo wote kuwafuja Mambo huwenda kwa daraja ya kufuata shar iya Pili anatoa kauli na mawaidha: ( 4) Sikiza yangu kauli Nisai na marijali aso hill ana hili wako wema na wabaya Kwa k-weli suluhisho lake la kutatua matatizo hayo ya ndoa :ni sawa sawa na suluhisho la Mukhlisa: ( 5) lnapasa kusubiri Na alojikwa na shmi asa itakuwa kheli Rabi atamwondasheya Naye Sheykha Bint Sheikh wa Kilifi huko Kenya pia anatoa mawaidha hayo gazetini hnmo, mnamo 22 Juni, 1956, wiki moja baadaye: ( 14a) Ilobaki kusubir i na kushukuru Jabari lakini hayo ni shtihizai ('iiony') tu, kwani katika ubeti ule ule anaendela kuwaonya waume: (14b) Takaneni muaziri Mungu atatulzpia Utenzi wake wenye beti 17 ameuita 'Waume Zingatieni, Wake Mnatuonea' Isipokuwa anamwita Bi Moza 'Binti mwenye fahamu', kumtaka radhi na kumwomba usahibu wake, anamtetea Mukhlisa kwa moyo wote na kuwashambulia waume m~ja kwa moja, bila pingamizi yoyote: (8) Daima mwatutukana Mazungumzo hamna Anawaambia wanaume waliojibu: waume mkikutana ila wake jamia 2 Wakati wa k:uhariri na k:utayarisha makala hii kwa uchapishaji nimeshayapata (rhs)

6 RIDDER SAMSOM (7) Huku si kujibishana Ikiwa ni kutukanwa mwataka adhinana msai tushazoea Jinsi walivyotahamki anafananisha na rikodi: (9) Kula siku mwaabiri Hata mwisho santuri ya sir i na ya dhahir i imekwisha kutolewa Anaishia utenzi wake ambao haukuficha maoni yake na knwa na lugha kali, kwa knmwomba Moza Ali usahibu wake na 'ma;ibu kunetea' (maana yake: knniletea). Basi ilichukua mpaka toleo 1ililofuatia la 29 Juni, jawabu ya Moza Ali kntokea Mma hii katika beti zake ll hakmnshambulia Mukhlisa tena, alionyesha huruma zake kwake na knmwelewa shida zake: (3) Kwa hakika ana dhiki Ndipo alipohamaki kwa mume kumhiliki akaanza kupoteya Rata hivyo anmudiamdia maoni yake ya 'Mukhlisa nakuwasa' kwa vile anaona bora knmwingilia yule tu aliyemkosa Mukhlisa na sio waurne wengine ambao ni wacha Mungu. Lakini anaknbaliana na Sheikha binti Sheikh knwa: (8) Walojipa uhodan Wao si watu wazur i kutwimba kwa santuri bar a kuwanyamazia Na ndivyo anavyojaribu mwishowe katika utenzi wake, knutuliza ugomvi uliotokea katika majadiliano yote: (10) Bz Shekha kuambizana Na Ilahz Subhana ni sifa ya kupendana sana ametuusiya Bas~ majadiliano yalitulia kidogo kwa muda wa wiki saba mpaka katika matoleo ya tarehe 17 na 24 Agosti utungo wenye beti 35 ulichapishwa katika sehemu mbili. Haukuwa utenzi tena, mara hii iliknwa katika umbo la nyimbo (mishororo mitatu}. Mshairi anajiita kwa jina la knwatisha watu Ibni Shani Anamtetea Mukhlisa sana, knmwita 'mwanangu' na knsema knhusu waume: (2) Si haki waliotenda Nawaacha wataranda Naona mambo yapanda naona wamuonea hasema watamwachza bora naona kungzya Sehemu kubv.ra ya ny1.nbo yake yenye jina '}.Jv,;anan~.l kurnuonea hadi naunzia sand inaeleza kisa kirefu kuhusu mwanamme mmoja aliyeibiwa pesa na kijana mmoja aliyeknwa karibu naye Kwa kweli, kisa hiki kinaweza kikawa ni fumbo Inategemea msikilizaji anataka knelewa vipi na knfumbua kwa namna gani: inaelekea hizo pesa si pesa bali ni mkewe Lakini huyu aliyeibiwa yumkini ana mpenzi pia. Kwa kwe~ ni mafumbo, yaani Ibni Shani anataka knwaambia watu knwa wanawake kwa wanaume wakigombana ni kwa sababu wana wapenzi? Hatuj~ lakini tunayojua ni utetezi wake wa Mukhlisa: (20) Binti Mukhulisiya kwa hapa nampa njiya Na kama yawachukiya mwanangu nimpendaye neno baya awambiye hapo ni nymyi na mzye

IUNGO ZA KUJIBIZANA 7 Al Mukhlisa an~jibu tarehe 7 Septemba. Hagusi tena mada ya wake kuonewa na waume Anamshnkuru tuna kumkarabisha Ibni Shani, ambaya anamwita 'Mpenzi Baba Yangu' (2) Zako nyingi shukrani Kuja ukaniauni kwa wema na ihsani vita vilipozongea Anatubu kwa kuanzisha hivi vita na kujitetea: ( 18) Nasaha nilisikiza Hufikiri nikiwaza nikakaa kanyamaza mbona wananionea Baada ya jawabu hii ya Mukhlisa bado tungo ziliende1ea kuingia na kuchapishwa. Nayat~ja tu majina yao (pamoja na tatehe): 21 Septemba: 12 Oktoba: 19 Oktoba: 2 Novemba: 'Ukisema Ukisaza, Yangu Ninakuusiya' 'Ni Bora Ukatuliya, Sijitiye Mshawasha' 'Msitafote Udhiya, Nawawasa Nyamazeni' 'Ilahi Rabana, Tanihukumia' Nini imetokea katika tungo zote hizo za ~jibizana? Kwanza mshaiii mm~ja aliyejiita Al Mukhlisa ametupa chambo na kutazama samaki gani wata~ja kutafuna.. Ndoana ilikuwa ni kali sana Aliyozungumzia, wake kuonewa na waume, ni ya1e yaliyowafikia wanawake wengi na kujadiliwa sana wakati u1e huko Zanzibar, kama ilivyoonekana pia katika makala mbalimbali zilizotokea katika gazeti lile lile. Kati ya samaki waliokuja kutafuna chambo, Bi Moza Ali anachukua nafasi muhimu. Si kwa sababu ya tenzi zake tu na siasa yake kuwaelekea wanaume kwa wanawake wanaojibizana, lakini pia kwa vile wengine wanavyomtaja na kumsemesha. Katika kujibizana yeye akawa muhimu kuliko Mukhlisa mwenyewe kwa kiasi ambacho tunajiuliza kuwa, huyo siye Mukhlisa mwenyewe? Si mtindo tu anavyotunga Mukhlisa ambao unatudhanisha ndiye. Vile vile mwenyewe Bi Moza anatoa ushahidi kidogo mara ya kwanza anapoingia katika kujibizana kwa kumwambia Shekh Awsedi: 'umetujia kwa vigudi' Yumkini anachukua nafasi ya wake kwa jumla, lakini katika utenzi wake mwengine anamwambia Sheikha binti Shekh: 'Mukhlisa ni mwenzangu, lake yeye ndilo langu' Ikiwa kweli kama tunavyofikiii Bi Moza mwenyewe ndiye chanzo cha majadiliano, basi mashindano hayo si kwa ajili ya kushindana tu, lakini ni njja au, tuseme, mtindo wa kuwekea dhamiia ('theme') jukwaani kwajamii Katika uainishaji wa ushaiii wa Kiswahili wasomi kadhaa wamejatibu aina mbalimbali za matumizi ya tungo ziunganishwe na mada zinazozungumziwa katika hizo tungo. Ibmhim Nom Shariff ( 1983) ameainisha namna tano za matumizi: tungo za maoni ya kifalsafa, za kuhadithia, za mafunzo, za dua na za mawasiliano Lakini katika mfano wetu mmoja tu wa kujibizana tumeona kwamba mambo hayo yote matano yamo: maoni, kisa, mafunzo, dua na mawasiliano Wasomi wengi wengine wam"jmibu amdhi mbalimbali za tungo ziwe zihusiane na yaliyomo katika tungo au lengo lake W anaeleza kwamba tenzi zingefaa dini na hadithi r efu, mashaiii yangetumika kwa siasa au mawasiliano, nyimbo ziwe kwa harusi au ngoma. Hapa tumeonyesha kuwa fani mbalimbali za amdhi zimetumika kwa kujibizana Vile vile mitindo mbalimbali ya kifasihi inavyochambuliwa na lbrahinr Noor Sharif inatumika yote pamoja wakati mmoja:

8 RIDDER SAMSOM mtindo wa moja kwa moja ('plain style'), tashbiha ('simile') na sitiati ('metaphoric style'), na mafumbo ('Iiddle style') Katika makala yake kuhusu vijembe kwenye kanga 'The Power of Incompleteness: innuendo in Swahili women's dtess' (1996), David Parkin anajiuliza kwa nini aina ya matumizi ya 1ugha kama hii ina nguvu sana. Mtu akitaka mwenzake kumsikiliza hatumii lugha ya kila siku Akitaka kumshawishi mtu au kusisitiza jambo fulani hutumia lugha maalum yenye mitindo maalum, hutumia lugha yenye nguvu Anasema Patkin: 'Perhaps it can be suggested that the "violent" uses of innuendo most likely typify rhetorical persuasion and the more pacific and evocative uses inform poetics.. But even this comes close to yet another dangerous tautology and one suspects that the problem here is, indeed, that rhetoric and poetics have been defined as separate discomses rather than as arbritrarily de:fi)led bundles of overlapping tendencies within discomse' Ushairi wa kujibizana unaonyesha hayo matumizi maalum makali ya lugha yanavyotumika pia katika vijembe. Madhumuni yake ni haja ya kutaka kushawishi, ushawishi ('persuasiveness'). Lakini mashindano hayo si kushindana, bali ni kuwasiliana, kulmnbana, kujadiliana pamoja na kukinzana Ni kuambizana, na, asemavyo Moza Ali, ni kupendana MARE leo Assibu A Amidu 1990 Kimwondo A Kiswahili electmal contest Wien: Beitriige zur Afiikanistik K Anui Abedi. 1954 [repr 1979] Shena za kutunga mashairi na diwani ya Amri. Nairobi: Kenya Literatme Bmeau. Hanies, Lyndon 1963 Swahili poetry Oxford: Clarendon Press Hanies, Lyndon 1966. Poems ftom Kenya Gnomic ver~es in Swahili qy Ahmad Nassir bzn Juma Bhalo. Madison, Milwaukee, London: University ofwisconsin Press. lbrahim Noor Shariff 1983. The function of dialogue poetry in Swahili society PhD dissertation Rutgers University, New Jersey. Ann Arbor: University Microfilms Jbrahim Nom Shariff. 1988 Tunga zetu. Trenton, N J.: The Red Sea Press Knappelt, Tan (ed ). 1964.. "Adhabu za Jahanuamu" Swahili Journa/34,1 Mulokozi, MM and I SY Sengo 1995. "History of Kiswalrili poetry [AD 1000-2000] " University ofdat es Salaam: OSSREA/IKR Mwongozi Mei- Nov 1956 Zanzibat: Ahmed S Kharusi Parkin, David. 1996 "The power of incompleteness: innuendo in Swalrili women's dtess." Anth1opologie de l'inte!locution. ed.. by B Masquelier and Jean-Louis Siran. Paris: l'harmattan [Forthcoming] Shaaban Robert 1991 [repr.] Maisha yangu na baada ya miaka hamsini.. Dat es SalaaiU: Mkuki na Nyota

TUNGO ZA KUJIBIZANA 9 NYONGEZA: kutoka gazeti la Mwongozi Voll5 No 17, p 6, 25 Mei 1956 W ANAW AKE IUF ANYEJE? I Bismillahi awali nanena yangn kauli Waume wenye akili wameihama dunia 2 Wameihama dunia Wanaojua sharia Hapa waliobakia ni wengi wenye udhiya 3 Sharia hawaijali nikaha hawaibali Wake wawatupa mbali waandama yao njia 4 Nyumba wanazipuuza wake wanawachagiza Hawawezi kutimiza ahadi walizotoa 5 Wake wakizaa nao watoto huwa ni wao Kwajina si kwa kivao wala si kwa kutumia 6 Hasa waume wa Ieo ati hat a wenye eh eo Hugeuka vipepeo kuruka wakakimbia 7 Lipi linowakimbiza waume wetu nawaza Wake wanawaliwaza nyumbani mkiingia 8 Majibu yatushangaza jambo linowakimbiza Ni haki kutekeleza na kukabili shaiia 9 Wanawake masikini wametuliza makini Wajitahidi yakini yao yawaendea 10 Kwani huitafuta kazi wakajivisha kivazi Wakawalipa walezi na watoto wao pia 11 Kifika mwisho wa mwezi h~jitia ubabazi Waume hawasikizi lo lote utowambia 12 Ramadhani 'kiwadia ukali wanajitia Huna la kuwaambia wakaibadili nia 13 Sikukuu jambo moja Zakaa inawangoja Watatoa kila hoja ya kukimbia sharia 14 Wake wakilalamika maja wapewa talaka Watoto na kuwataka kama waliwalipia 15 W akiwacha wake zao pamoja na wana wao Husahau haki zao watoto kuwangilia 16 Mtoto hutoka jasho akenda kutaka posho Njoo Ieo njoo kesho huzungnshwa kama pia 17 Wake wanaponyamaa waume huchachawaa W akinena huwa baa mpaka kupindukia

10 RIDDER SAMSOM 18 Mradi hayasemeki W anawake wana dhiki 19. Sasa yaliyobakia Mungu tatusaidia 20 Iuwe wana wa subiia Mola atupe ijara waume wanahiliki wan~juta kuolewa ni duwa kujiombea tuzidi kuzingatia tukenda kesho akhera aliyotuandikia Al-Mukblisa