KANISA LINAHITAJI KUJUA



Similar documents
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA BILL SUPPLEMENT

TUNGO ZA KUJIBIZANA: "KUAMBIZANA NI SIFA YA KUPENDANA"t

MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

Contents Page. 3. Financial Highlights 4-8. Chairman s Statement CEO s Statement

Annual Report and Financial Statements

Ni Wakati Wa Kuamka! Ellis P. Forsman. Ni Wakati Wa Kuamka (It's Time To Wake Up) 1

THE OIL AND GAS REVENUES MANAGEMENT ACT, 2015 ARRANGEMENT OF SECTIONS PART I PRELIMINARY PROVISIONS PART II ADMINISTRATIVE PROVISIONS

Linking Adult Education with Formal Schooling in Tanzania: Mission Unfulfilled

TANZANIA COFFEE BOARD VACANCIES ANNOUNCEMENT

Contents. CORE VALUES Integrity Professionalism Team Spirit Safety Culture. Company Information 2 Message from the Chairman 4

MARX'S SHORTS AND ANCESTORS' CAVES: TRACING CRITICAL MOTIFS IN KEZILAHABI'S PLAY AND POEMS*

TANZANIA AND HIV/AIDS TANZANIA NA UKIMWI

Je! Mungu Habadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

Ndugu na dada zangu. Mbio za Maisha

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Januari, 2015

EXISTENTIALISM AND FEMINISM IN KEZILAHABI S NOVEL KICHWAMAJI

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION CKRC VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, SABOTI CONSTITUENCY, HELD AT KITALE TOWN MUSEUM HALL

Lesson 56: Business: [biashara: ununuzi, upigaji bei na uuzaji] Business: Shopping, Buying and Selling. A). Business Vocabulary.

Annual Report Report and and Financial Statements

ROMAN CATHOLIC FAITH REPRESENTED IN KEZILAHABI'S MZINGILE SONJA MEZGER AAP 72 (2002) SWAHILI FORUM IX 75-85

DAR ES SALAAM UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION. A Constituent College of the University of Dar Es Salaam STAFF FUNERAL POLICY

OPERATIONS MANUAL FOR IMPLEMENTATION AND MANAGEMENT OF A COMMUNITY HEALTH FUND in Tanga Region

Creation of a Speech to Text System for Kiswahili

Centum Investment Company Limited Annual Report & Financial Statements fy 13/14

Lesson 14a: Numbers and Counting

KUKITANDAWAZISHA KISWAHILI KUPITIA SIMU ZA KIGANJANI: TAFAKARI KUHUSU ISIMUJAMII

Kitabu hiki kimefanikishwa kwa msaada wa Taasisi ya Bill na Melinda Gates

815 SWA. Health undertaking Kuwajibika Kiafya. Tafadhali weka kurasa hii ya maelezo kama kumbukumbu yako

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,

Yaliyomo. II. Dodoso la Kilimo... 62

Uundaji wa Istilahi za Kiswahili Kileksikografia na Athari zake S.S. SEWANGI University of Dar-es-Salaam, Tanzania

THE ANTI-MONEY LAUNDERING ACT,2006

CONTENTS. Financial Section. Sehemu ya Kiswahili. Statutory Information

Tunza Jamii Yako, Tunza Mazingira Yako kwa Maisha Bora. Jihusishe. Jipangie. Amua

MWONGOZO WA USHIRIKISHWAJI KATIKA KUPANGA MATUMIZI YA ARDHI WORLD BANK

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF

CUF. Rais makini, Serikali makini Uchumi Imara, Mabadiliko Sahihi

Mwalimu Nyerere Engages His People: Scripture Translation in Swahili Verse

ANNUAL REPORT 2015 THE TASKS OF TBL INTRODUCING

TEGENI MASIKIO: COMPOSING EAST AFRICAN REALITIES THROUGH YOUNG EYES

A SHABA SWAHILI LIFE HISTORY: TEXT AND TRANSLATION

LEARNING HOW TO TEACH

Tuko Pamoja. Adolescent Reproductive Health and Life Skills Curriculum

TAARIFA YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA UKIMWI MKOA WA KIGOMA

Language Choice in Swahili Newspaper Advertising in Tanzania

LUGHA YA MITAANI IN TANZANIA THE POETICS AND SOCIOLOGY OF A YOUNG URBAN STYLE OF SPEAKING

Sda Church Nyimbo Za Kristo

MORE SWAHILI PROVERBS FROM EAST AFRICA METHALI ZAIDI ZA KISWAHILI TOKA AFRIKA MASHARIKI. L. Kalugila. A. Y. Lodhi

HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII MKOA WA DODOMA

The Usage of Kiswahili in Blog Discourse and the Effect on Its Development

Lesson 24: Adjectives

CURRICULUM INNOVATION IN TEACHER EDUCATION

Celebration of the French «Bastille Day» Remarks by Ambassador Elisabeth Barbier 14th July 2010

KISWAHILI Pam Inoti - pamby22@gmail.com

P.O. Box 4374 DAR ES SALAAM TEL: /6 FAX:

TRAINING ON ENTREPRENEURSHIP AND BUSINESS MANAGEMENT SKILLS FOR SELECTED VILLAGERS IN RUFIJI

Teach Yourself Swahili

The mother, her confidants and the prevention of mother-to-child transmission of HIV (PMTCT) services in the Kilimanjaro region, Tanzania

DR. HAMISI O. BABUSA (PHD)

Promoting Regional Trade to Enhance Food Security

MEANING AS USE: A FUNCTIONAL VIEW OF SEMANTICS AND PRAGMATICS

Ambassador s Community Grants Fund for HIV/AIDS Relief

ARMS CONTROL Volume 3 Issue 1 May 2011

Mother Tongue Theological Education in Africa: A Response to Jim Harries The Prospects for Mother Tongue Theological Education in Western Kenya

1. TASAF operations steadily approaching set targets

TEKNOLOJIA ZA UTAYARISHAJI, USINDIKAJI NA HIFADHI YA MAZAO YA MBEGU ZA MAFUTA BAADA YA KUVUNA. Kitabu Namba 5

Swahili. Information provided by: National African Language Resource Center (NALRC)

CURRICULUM VITAE PERSONAL DETAILS. Prof. Wanyama Mellitus Nyongesa. Age: 47. Associate Professor of Musicology at Moi University, Eldoret, Kenya

Winners, cheats and witches: East African soccer cartoons Beez, Jigal

Lesson 43: Commands. D). Commands may take object markers to indicate the recipient of a command

Schneps, Leila; Colmez, Coralie. Math on Trial : How Numbers Get Used and Abused in the Courtroom. New York, NY, USA: Basic Books, p i.

The Mosaic Project Theme Song 2001 The Mosaic Project Music by Brett Dennen, Lyrics by Brett Dennen and Lara Mendel

Girls Getting to Secondary School Safely: Combating Gender-based Violence in the Transportation Sector in Tanzania

The United Republic of Tanzania

NEGOTIATING THE NEW TUKI ENGLISH-SW AHILI DICTIONARY A CRITIQUE FROM A PEDAGOGICAL AND SCHOLARLY PERSPECTIVE'

Section 2 Assessment

INITIAL BEHAVIOR CHANGE COMMUNICATION (BCC) INTERVENTIONS EFFECTIVENESS EVALUATION REPORT


Towards Full Comprehension of Swahili Natural Language Statements for Database Querying

TANZANIA PARALEGAL BASELINE SURVEY

L E A P n e w s. Tahariri. Editor s note. Number 15/16 September December 2007 Newsletter of the Language in Education in Africa Project

ACADRI 2015 TRAINING PROGRAMMES

Integrated Logistics System (ILS) Procedures Manual

The Nguzo Saba of the seven days of Kwanzaa:

The Story of Swahili

Your Rights and Responsibilities

ก ก ก ก Hydrologic Cycle

LIN892: Distributed Morphology


CURRICULUM VITAE. 1. SUMMARY OF EXPERIENCE Special Needs Education Lecturer Psycho-educational Assessment Professional

Lesson 9: Swahili Noun Classes

Primary Care Plus Enrollment Booklet

V-TO-I MOVEMENT IN KISWAHILI

MOSHI UNIVERSITY COLLEGE OF CO-OPERATIVE AND BUSINESS STUDIES (MUCCoBS) A Constituent College of Sokoine University of Agriculture



Tense and aspect in Swahili

Vidunda (G38) as an Endangered Language?

Lourenco Noronha. Lektor ( für Swahili Literatur am Institut für Afrikawissenschaften der Universität Wien

ORODHA YA TAASISI/MAKAMPUNI

Transcription:

Miki Hardy KANISA LINAHITAJI KUJUA Umefika wakati tuyazungumzie mambo kadhaa ya msingi waziwazi ili Wakristo watambue ya kwamba Bwana ana mambo mazuri zaidi kwa ajili yao!

Hakimiliki 2013 na Church Team Ministries International (CTMI) Kanisa Linahitaji Kujua na Miki Hardy. Imechapishwa na Church Team Ministries International (CTMI) Toleo la kwanza: Julai 2015 Jalada limebuniwa na: Idara ya Habari ya CTMI Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho hili inayoweza kunakiliwa, kusambazwa,au kutolewa kwa namna yo yote ile isipokuwa kwa ruhusa ya mchapishaji. Vifungu vya Biblia vimetolewa katika Biblia, Swahili Union Version, 1962. Machapisho mengi ya Church Team Ministries International yanapatikana kwa gharama nafuu ikiwa yananunuliwa kwa jumla kwa ajili ya kutangaza, kuchangisha fedha, kugawa bure, na kwa kuelimishia. Kwa maelezo zaidi, tuandikie: Media Dept., CTMI, Trianon, Mauritius; au tuma baruapepe kwa: media@ctmi.org Tembelea tovuti yetu: www.ctmi.org ISBN 978-99949-0-181-4 10

Yaliyomo I. Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka... 5 II. Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo?... 15 III. Mkristo na Pesa... 23 IV. Mungu na Muziki... 31 V. Vita ya Rohoni... 39 VI. Mahusiano Kabla ya Ndoa... 47 VII. Barabara ni Nyembamba... 55 VIII. Kanisa Litakabiliwa... 65 IX. Yesu Anaita Tena... 75 3

4

Sura ya I Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka 5

Wakristo wengi leo wanaweza kukumbuka wakati ambapo suala la talaka kwa mchungaji au kiongozi wa Kanisa lilikuwa ni jambo la aibu isiyoneneka. Hapakuwepo na uwezekano kwa mtu wa jinsi hiyo kuendelea katika utumishi. Zaidi na zaidi, leo tunaona wachungaji wakitoa talaka, wakioa upya na kuendelea na huduma kana kwamba hakuna jambo zito lililofanyika. Ninaamini haya ni matokeo ya anguko na udini ambavyo vimechukua nafasi ya fundisho la uzima na Kweli ya Kibiblia ndani ya Kanisa. Hili ndilo chimbuko la hii hali ya mambo. Sasa, ikiwa mchungaji anaweza kumpa mkewe talaka na akaendelea kuwaongoza watu wa Mungu, je! waumini wanapata mfano wa jinsi gani wa kuiga? Labda maswali tunayopaswa kujiuliza ni, Ni kwa nini Wakristo wawili waliojazwa Roho Mtakatifu washindwe kutatua tofauti zao na, Je! kuna uhalali wo wote kwa haya matatizo kutotatulika, au kwa wawili hawa kuachana? Ama liwe linamhusu mchungaji, au mshirika wa kanisa, ninaamini suala la kutengana, kutoa talaka, na kufunga ndoa mara ya pili hufanyika kwa sababu hawa watu hawajui wajibu wao kamili mmoja kwa mwingine katika ndoa. Tunaona kwenye Maandiko ya kuwa mume ana wajibu mkubwa mno: kumpenda mkewe kama Kristo anavyolipenda Kanisa. Vivyo hivyo, mke naye ameitwa amtii mumewe. Kama wawili hawa wasipouchukua msalaba wao, na kumruhusu Roho wa Mungu awavunje na kuwabadilisha, hilo kamwe halitakuja kutokea Mungu peke yake ndiye anayeweza kulifanya hili mioyoni mwao. Hakuna mbinu inayoweza kulifanya hili ni matokeo ya kazi ya Msalaba maishani mwao! 6

Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka Sijaona popote kwenye Maandiko kinachonielekeza kuamini ya kuwa ni mapenzi ya Mungu kwa wanandoa Wakristo, achilia mbali mchungaji, kutoa talaka. Hii ni kwa sababu Mungu, kwa njia ya Msalaba, ameleta njia ya kurejesha upendo na umoja kati yao. Hebu sasa tuangalie Neno la Mungu linavyotufunulia kuhusu suala la ndoa na talaka Siku hizi, watu wengi hawaoni shida kwa Wakristo wanandoa kuachana kwa sababu tu mmoja wao hapatani na mwenzake; au kwa kuwa tu hawana mtazamo mmoja kuhusu mambo mbalimbali au hawana tena maono mamoja! Hakika hili ni eneo ambalo Kanisa limekubali kuathiriwa si tu na njia za ulimwengu usioamini, bali pia na viongozi wa Kikristo ambao wameandika vitabu, wakihalalisha matendo yao ya kibinafsi sana na ambao, kwa kuamua kuchukua njia ya talaka wamefungua mlango kwa waumini kufanya vile vile. Ninaamini ya kwamba badala yake, tunapaswa tuuangalie mtazamo wa Mungu juu ya suala hili. Ndoa Kwenye Agano Jipya Kwenye kitabu cha Mwanzo, Mungu aliianzisha ndoa. Baada ya yale Yesu aliyokamilisha Msalabani, ndoa ya kwenye Agano la Kale, yenye wake wengi na hati za talaka, haiwezi tena kulinganishwa na ndoa chini ya Agano Jipya. 7

Mpango wa Mungu kwetu sisi, kama Wakristo tuliozaliwa mara ya pili, ni kuishi na waume zetu na wake zetu hadi kifo kitakapotutenganisha. Katika Marko 10:2, kwa kuwa Yesu alikuwa akiwahoji Mafarisayo juu ya mtazamo wao wa kisheria katika masuala mengi, walimjaribu kwa kumwuuliza: Je, ni halali kwa mtu kumwacha mkewe? Yesu akawaonyesha ya kuwa, chini ya Musa na Torati, Mungu aliruhusu talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao (Marko 10:5); lakini katika Agano Jipya, mambo yangekuwa tofauti. Katika Mathayo 5:32, anazungumzia waziwazi juu ya kile kinachotarajiwa kwa waamini wote wa Agano Jipya: Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. Isipokuwa kwa habari ya uasherati bila shaka haimaanishi pale mwenzi mmoja anapoanguka katika dhambi na kufanya tendo moja la uasherati au la kukosa uaminifu. Inazungumzia mtu ambaye amerudi nyuma na anaishi katika dhambi, na aliyedhamiria kuendelea kuishi katika dhambi. Kwa kuiruhusu talaka katika mazingira hayo maalum, Yesu hajaondoa ukweli kwamba yule aliyekosewa bado anatakiwa kunyenyekea na kusamehe. Hili linaweza kufanyika kwa dhati pale tu tunapoikubali njia ya Msalaba. Kwa hivyo, Biblia iko wazi: kwenye Agano Jipya, hakuna uhalali wowote wa kutoa talaka isipokuwa katika maeneo maalum sana vinginevyo itapunguza kile Yesu alichokifanya Kalvari! 8

Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka Injili Zisizokuwa Na Uweza Nina hakika utakuwa umegundua ya kuwa Kanisa limepoteza mwelekeo katika hili eneo, na linaenenda kama vile Injili ni kitu kinachobadilika kwa kutegemea nyakati. Katika miongo michache iliyopita, Kanisa, kwa kujumuisha wachungaji na viongozi, kwa usahihi kabisa, halikukubaliana na talaka, lakini leo hii talaka imekubalika makanisani. Ni nini kilichofanyika? Bila shaka ni kwa sababu injili inayohubiriwa leo hii imebadilika na haina uwezo wa kushughulika na mambo ya jinsi hiyo. Haina nguvu tena ya kuihakiki dhambi kama mwanzoni. Mfano mzuri ni injili ya Mafanikio inayovuta mioyo ya watu kuyaandamia mambo ya mwilini badala ya kutafuta makuzi ya rohoni. Haijengi, na hakika haina uwezo wa kukabiliana na mambo ya ndani ambayo Wakristo wanapambana nayo leo. Hii ndio maana ni muhimu turejee kwenye injili ya ufunuo wa Msalaba ikiwa tutataka kuona familia za Kikristo zenye umoja pamoja na kupungua kwa kiwango cha talaka Kanisani. Siku hizi Wakristo mara nyingi wanataka njia rahisi ya kutatua matatizo yao ya ndoa, mlango rahisi wa kutokea. Wanaachana kwa sababu nyepesi kama vile: Mke wangu hanitii ; Mume wangu si mtu wa rohoni, au mbaya zaidi, Hatupatani tena, maono yetu na matarajio yetu yamebadilika Watu wa jinsi hii bila shaka hawajaisikia injili sahihi, kwani injili sahihi itawaongoza katika kuwajibika kila mmoja kwa mwenzake. 9

Nafasi Ya Mume Niruhusu nifafanue juu ya ufunuo wa ajabu Paulo aliopewa kuhusu ndoa kwenye Waefeso 5. Uhusiano wa mume na mke ndio tu uliolinganishwa katika Agano Jipya na uhusiano Yesu alio nao na Kanisa lake. Paulo anatamka kwa ujasiri ya kuwa, KAMA Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake VIVYO HIVYO mume naye anapaswa kumpenda mke wake. Yesu alijinyenyekeza, akachukua sura ya mwanadamu, akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Hiyo ndiyo hali ya moyo Yesu anayoagiza mume awe nayo kwa mke wake. Huo ndio wajibu wa mume: kama Yesu, yeye naye anaitwa apoteze haki zake na autoe uhai wake kwa ajili ya mke wake. Huu ndio ufunguo wa ndoa yenye mafanikio. Utaratibu Wa Mungu Kwenye Ndoa Nafasi ya mke imefananishwa na ile ya Kanisa. Paulo anatamka ya kuwa KAMA vile Kanisa limtiivyo Kristo, VIVYO HIVYO mke naye anapaswa kumtii mumewe. Kwa hivyo, Kanisa wewe na mimi linapoelewa kile Yesu alichofanya msalabani kwa ajili yetu; kwa maneno mengine, upendo aliouonyesha, sisi nasi tunaweza kumpenda pia. Isingewezekana tumpende Yeye kabla ya kuujua upendo wake kwetu. Je, unaweza ukaona utaratibu wa mambo hapa? 10

Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka Ni wazi, basi, kwamba mume ana wajibu mkubwa zaidi kuliko mke katika ndoa, kwani huduma yake inalinganishwa na ya Kristo, ilhali ya mke imefananishwa na ya Kanisa. Ikiwa mume atakuwa tayari kuchukua hatua ya kwanza, katika kuutii wito wake, kama Kristo alivyofanya, moja kwa moja atavuna hali ya utii kutoka kwa mke wake. Katika mazingira ya kawaida, hatutarajii kwamba utii wa mwanamke kwa mumewe utakuwa wa moja kwa moja; lakini msingi sahihi unapokuwepo, mume anaweza akatarajia ya kuwa mkewe atamnyenyekea. Hata hivyo, hata kama mke hatafanya vile, mume anapaswa aendelee kuyatoa maisha yake kwake, na amtegemee Mungu kufanya muujiza moyoni mwa mkewe. Mwishoni mwa kifungu hiki, Paulo ananukuu andiko kutoka katika Agano la Kale, Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Moyo wa Mungu kwa ajili ya ndoa ni mume na mke wadumu katika umoja maisha yao yote. Tunapozitii amri za Mungu, yeye ni mwaminifu na hutenda miujiza. Mume Wa Mke Mmoja Yapo mambo mengi sana yahusuyo ndoa ambayo hayajatajwa katika Biblia. Kanisani mwetu penyewe tumeshuhudia matukio mengi tofauti katika miaka hii mingi, na tumejifunza kuyatatua kila moja kwa namna yake, katika neema na kweli. Mahali ndugu wa kiume au wa kike alipoichukua njia ya Msalaba, na kuiruhusu toba kufanya kazi 11

moyoni mwake, tumeshuhudia urejesho na ushindi maishani mwao na katika utumishi wao kwa Bwana. Na hebu niongeze kusema ya kwamba Mungu si Mungu anayetoa nafasi ya pili au ya tatu ya kujaribisha mambo. Mpango wake sikuzote ni kwa mume kuwa na mke mmoja, na ametuwezesha katika hilo kwa kumtuma Yesu katika mfano wa mwanadamu, afe Msalabani na kuishinda dhambi katika mwili. Ni juu yetu kuyatoa maisha yetu yawe dhabihu ili miili yetu isulubiwe. Mwanamume anayemwacha mkewe halafu akaendelea katika utumishi kana kwamba hakuna kilichofanyika, hawezi kutarajia kuendelea kubeba upako ule ule katika utumishi wake kwa Bwana, na hasa ikiwa ameoa tena, hadi atakapoacha kuhalalisha uamuzi wake huo na kutubu. Ufunguo Unaoleta Matengenezo Si mpango wa Mungu kwa mtu yeyote kumwacha mwenzi wake. Mungu anachukia talaka; lakini hawakatai wale walioachana au waliooa ama kuolewa mara ya pili ikiwa watatubu. Ikiwa nimegusa eneo linalokuhusu, hujachelewa. Mungu anaweza kukurejesha, pamoja na utumishi wako kama uko kwenye huduma, ikiwa utakuwa tayari kukiri ya kuwa haukuenenda sawasawa na moyo wala Neno la Mungu, bali ulifuata tamaa za mwili wako; na ya kuwa, inawezekana ulijiingiza katika mahusiano yasiyo sahihi. 12

Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka Ikiwa ni hivyo, ni lazima umrudie Bwana kwa toba ya kweli; kulingana na maongozi ya Roho Mtakatifu, na ukiwa na utayari wa kufanya lolote atakalokuagiza kufanya... hata kama itakulazimu kumrudia mwenzi wako wa mwanzo. Kumbuka ya kwamba Bwana hahitaji sababu au maelezo kuhusu mwenzi wako, au kuhusu yale aliyoyafanya. Yeye huuangalia moyo wa mtu. Katika kila jambo, Mungu anatamani tuwe na moyo safi, mnyenyekevu, uliojaa msamaha, na ulio na toba. Inawezekana yakawepo mahusiano ambayo pengine hayawezi kurekebishika; ila, mengi zaidi yanarekebishika, ikiwa tuko tayari kujikana nafsi zetu na kuuchukua msalaba wetu. Msalaba ndilo suluhisho la Mungu kwa ndoa yenye mafanikio! 13

14

Sura ya II Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo? 15

Katika safari zangu barani Afrika katika miaka 25 iliyopita, swali moja limekuwa likijitokeza mara kwa mara: Je, inawezekana kwa Mkristo aliyezaliwa mara ya pili kupagawa mapepo? Hili jambo mara nyingi huhusishwa na maisha aliyoishi mhusika huko nyuma, au kibaya zaidi, linahusishwa na mambo waliyoyafanya mababu zake. Inanihuzunisha kuona kwamba kuna Wakristo wengi wanaoamini ya kwamba wao, au ndugu zao wa kiume na wa kike katika Kristo wanaweza kupagawa mapepo baada ya kupokea wokovu. Sote tunakubali ya kuwa kazi za mapepo na roho chafu zipo. Lakini je! inawezekana kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili kuhitaji kufunguliwa kutokana na nguvu za mapepo? Ninaposoma Maandiko, jibu langu kwa swali hili ni Hapana! yenye nguvu. Biblia iko wazi kuhusu hili suala: tunapozaliwa mara ya pili, tunaokolewa kutoka katika nguvu za giza na kuingizwa katika Ufalme wa Yesu Kristo. Roho Mtakatifu anakuja kuishi ndani yetu na nuru haiwezi kukaa pamoja na giza. Hakuna jinsi kabisa ambapo pepo anaweza akaishi ki-kwelikweli ndani ya Mkristo aliyezaliwa mara ya pili, aliyeyatoa maisha yake kwa Bwana Yesu Kristo na anayetamani kumtumikia. Haiwezekani kabisa! Tunapaswa tuhoji wokovu wa watu waliojitokeza kwenye mikutano na kuungama sala ya toba, halafu wakaendelea kudhihirisha dalili za kupagawa mapepo. Katika hali kama hizo, labda tungepaswa kuuliza swali: Je, toba ya kweli imefanyika mioyoni mwao? Lakini cha muhimu zaidi, ni kwamba ninaamini matatizo mengi yanayosingiziwa pepo ni madhihirisho tu ya mwili. Kwa bahati mbaya, 16

Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo? Wakristo wengi wameaminishwa ya kwamba haya madhihirisho ya mwili ni kazi za Shetani. Jambo ambalo Kanisa linapaswa kujua ni kwamba, katika hali kama hizi, maombezi ya ukombozi sio jawabu. Maisha yetu yanapooana na mfano wa Yesu Kristo, na tunapouchukua Msalaba wetu kila siku, na kuifisha miili yetu na kumfuata yeye, suala la kupagawa pepo halitakuwa tatizo maishani mwetu, au kwa Kanisa. Ulimwengu wa roho upo na unaweza kuwa na nguvu kuliko tunavyofikiri. Ndio maana Mungu anapogusa maisha yetu tunaweza kubadilishwa mara moja. Kwa msingi huo huo kuna watu ambao maisha yao yameathiriwa na mapepo pamoja na roho za kishetani. Katika vitabu vya injili, Yesu mwenyewe alitoa pepo na kuwaweka watu huru. Ukweli kwamba watu wanapagawa mapepo upo na hauwezi kupingwa. Hata hivyo, katika Mathayo 12, Yesu anapozungumza juu ya kutoa pepo, alizungumza kabla ya Msalaba na alikuwa akizungumzia kizazi kikaidi, sio Kanisa. Kwa hivyo, swali langu ni hili: Wakristo waliozaliwa mara ya pili, waliotubu dhambi zao za kale, na kuyasalimisha maisha yao kwa Yesu, je! bado wanahitaji kufunguliwa kutoka katika nguvu za mapepo? Kuzaliwa Mara Ya Pili Au Kutokuzaliwa Kabisa Sijaona mahali popote kwenye Biblia Wakristo katika Kanisa la mwanzo wakitolewa mapepo. Ama umezaliwa mara ya pili au la; 17

hakuna zaidi! Kabla ya kumjua Yesu tulikuwa chini ya mamlaka ya Shetani. Hatukumjua Mungu; na sisi sote pia tulikuwa chini ya ushawishi wa roho za kishetani au tulitawaliwa nazo (Waefeso 2:1-5). Mtu asiyeamini anapotubu dhambi zake na kuamini katika dhabihu ya Yesu msalabani, Mwenyezi Mungu mwenyewe huja na kuishi moyoni mwake. Wakolosai 1:13 inaelezea hivi: Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake. Baada ya sisi kuzaliwa upya na Roho Mtakatifu, asili ya Mungu inachukua nafasi ya asili ya dhambi iliyotutawala mioyoni mwetu hapo kabla. Mara nyingi sio lazima hata kuomba ili mtu afunguliwe. Yule asiyeamini tayari yuko chini ya hukumu kubwa sana na yuko tayari kuyasalimisha maisha yake kwa Kristo, kiasi kwamba anawekwa huru kwa wepesi sana kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Mara nyingine anahitajika kufanyiwa maombi ili afunguliwe. Kutokana na hayo unaweza ukauliza je, maana yake nini haya madhihirisho ya nguvu za giza leo hii makanisani? Jawabu ni kwamba watu wengi huja tu kwa ajili ya kupokea uponyaji na kufunguliwa kutokana na nguvu za giza, kubarikiwa, na si kumtafuta Mungu kwanza. Na kwa sababu hawajazaliwa mara ya pili, nguvu za giza huendelea kuyatawala maisha yao. Lakini haiwezekani kwa Wakristo waliozaliwa mara ya pili kuendelea kuwa chini ya nguvu za mapepo, isipokuwa wamerudi nyuma hadi kuvunja kabisa uhusiano wao na Kristo, wamemkataa Bwana na kuzifungulia mlango kazi za mapepo mioyoni mwao na 18

Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo? maishani mwao. Kwa sababu, inawezekanaje Roho Mtakatifu kuishi kwenye mwili mmoja na pepo? Shida nyingi na mambo mengi yanayohusishwa na mapepo yana mizizi yake kwingineko. Kama hatupo kwenye msingi wa Msalaba tunajikuta tukipokea kila aina ya mafundisho ya uongo na imani za kigeni. Kwa kila jambo linaloharibika tunatupia pepo lawama. Ni Mwili! Ni lazima ieleweke kwamba ikiwa mimi kama Mkristo nina shida na mwili wangu, haina maana kwamba kuna pepo ndani yangu ila ni kwamba tu nimeziruhusu tamaa za mwili wangu zinitawale. Ni kweli twaweza kujaribiwa, lakini ni lazima tutofautishe kati ya kujaribiwa na kumilikiwa na roho chafu. Ni pale tu nitakapojikana nafsi yangu, kuwa tayari kuziachilia haki zangu na kuyapoteza maisha yangu kwa kuuchukua msalaba wangu, ndipo nitakapopata ushindi katika eneo husika. Sihitaji kabisa kukemewa pepo yeyote atoke, maana tayari niko huru na mapepo! 19

Maombi ya Kufunguliwa Sio Jawabu Mungu ametufungulia njia ya kutokushindwa na miili yetu, au kuzisikiliza tamaa zake. Ni Msalaba. Ndio maana maisha yetu hayana uhusiano wowote na mapepo. Roho wa Mungu anaishi ndani yetu. Yeye anatuombea na kutuwezesha, kwa neema ya Mungu, kuusulubisha huu mwili. Kile Mungu anachotaka kufanya maishani mwako kwa njia ya utakaso hakiwezi kupatikana kupitia maombezi ya kutoa pepo. Usimruhusu mtu yeyote ajaribu kukemea ndani yako pepo wa hasira, uvivu, wivu na kadhalika. Vivyo hivyo huwezi kutatua tofauti zilizopo kati yako na mwenzi wako, watoto wako au Mkristo mwenzako kwa kukemewa pepo... Haya ni madhihirisho ya mwili wako, matokeo ya maisha ambayo hayajasalimishwa kwa Bwana. Wakristo wengi leo wamekata tamaa kwa sababu wanafahamu ni aina gani ya watu wanaopaswa kuwa, lakini wanapoitazama hali halisi ya maisha yao, wanahisi tu kushindwa na kukata tamaa. Hivyo wanakimbilia kwenye kutolewa pepo. Ushindi upo katika Msalaba. Hebu kuwa na utayari wa kuyapoteza maisha yako na utaona matokeo yake... Tunaweza kuwa dhaifu katika maeneo mengi, lakini bado tukaudhihirisha uzima wa Kristo. Tumewekwa huru mbali na mapepo na tunaitembelea hiyo njia ya kuuelekea ukamilifu; Bwana apewe sifa! Kwa maelezo kuhusiana na kazi za mwili, angalia orodha iliyoko Wagalatia 5:19-21. Na hebu nikuambie, huhitaji kutolewa pepo ili uweze kutembea katika ushindi dhidi ya mambo haya. Chukua tu msalaba wako. 20

Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo? Kujifananisha Na Kristo Ni muhimu tuweze kuelewa kusudi la ujumbe wa Msalaba kwa maisha yetu. Ni lazima tuwe tayari kujifananisha na mauti ya Kristo ili tuweze kuubeba uzima wake na kuwa huru. Mara tu tunapouweka msalaba kando, tunatafuta njia za mkato, au jambo mbadala kama vile kukemewa pepo, yaani, aina ya Ukristo wa kubonyeza kitufe. Lakini katika Wagalatia 2:20, maneno ya Paulo, Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu ni tamko la ajabu linalodhihirisha aina ya maisha aliyoishi. Kupitia ufunuo alioupokea, Paulo alijifunza ya kwamba alihitajika ayafananishe maisha yake na maisha ya Kristo, ajikane nafsi yake, ausulubishe mwili wake. Aliuishi huo ufunuo na akaweza kuuhubiri; maisha yake yalikuwa ni ushuhuda wa mabadiliko yanayoletwa na kazi ya Msalaba. Ujumbe wa Msalaba ni onyo la mara kwa mara na kumbukumbu inayoufunua udhaifu wa miili yetu, na kutuwezesha kuona hali halisi ya maisha yetu. Inatuleta kwenye toba, kujikana nafsi na kurejea Msalabani. 21

Huru Kweli Kweli! Kwa hivyo, ndugu au dada mpendwa, ikiwa kutoka katika vina vya moyo wako umeyasalimisha maisha yako kwa Kristo, tofautisha kati ya udhaifu wa mwili wako na kupagawa mapepo. Unaweza ukawa ni Mkristo dhaifu, ila tambua umewekwa huru mbali na mapepo. Haleluya! Ndio sababu Mtume Paulo alinena sana juu ya hatari za mwili. Alifahamu fika udhaifu wa mwili. Kumbuka, Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli! 22

Sura ya III Mkristo na Pesa 23

Kama kuna eneo ambalo Wakristo leo hii wamelaghaiwa na kufundishwa mafundisho yenye udanganyifu, hakika ni katika eneo la fedha na utoaji. Ni aibu kubwa kwa Kanisa kuona wachungaji wengi wakilikosesha kundi la Mungu kwa kuwapa ahadi za uongo za mafanikio na baraka; wakiwapotosha kwa kutumia sheria zinazowashurutisha kutoa. Mara nyingi nimelishutumu fundisho la mafanikio lililolivamia Kanisa, kwenye nchi tajiri na nchi maskini. Jumbe zangu zimeelezewa kuwa zenye utata kwa sababu nimepinga kuhubiriwa fundisho hili la uongo. Sina tatizo kabisa Wakristo wanapotajirika kwa mali za ulimwengu huu, na wanapobarikiwa. Lakini ninapingana vikali na mafundisho ya kwamba ni mapenzi ya Mungu ya kuwa Wakristo wote wameitwa kuwa matajiri. Hili linapatikana wapi kwenye Biblia? Hata Kanisa la Mwanzo lilikuwa na Wakristo maskini. Kwa hivyo, ninaamini ni uzushi kuwaaminisha Wakristo wote ya kwamba ni mapenzi ya Mungu wote wawe matajiri, wote wamiliki majumba makubwa, magari ya kifahari, n.k., au ya kwamba wanapoendelea kubaki maskini ni kwa sababu hawana imani uzushi kabisa! Katika maeneo kama Afrika na India, Wakristo wengi wanaishi katika umaskini wa kutisha. Hakuna aibu katika hilo, na haimaanishi hawana imani. Zaidi ya hilo, katika mahubiri mengi ya siku hizi, pesa inapewa umuhimu kupita kiasi! 24

Sura ya III - Mkristo na Pesa Si kwamba ninalishambulia fundisho la mafanikio, lakini ninaamini tunahitajika tuangalie Neno la Mungu kuhusu hili suala katika mtazamo sahihi katika kuutafuta moyo wa Mungu kwa hili. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba waumini katika makanisa ambapo injili ya jinsi hii inahubiriwa, na ambao wengi wao ni maskini, hawafiki mahali pa kuelewa ya kwamba Mungu ana haja na aina ya moyo tulionao katika kumtolea. Mungu humpenda mtu anayetoa kwa moyo mkunjufu, si mtoaji tajiri! Katika makanisa mengi sana, linapokuja suala la utoaji, watu wanaleta sadaka zao wakitaraji kurudishiwa kwa wingi walichopanda, au kutokana na shinikizo na hofu ya kuonekana wanaenda kinyume na kile Biblia inachosema! Ila, tunapolitazama Neno la Mungu, je! ni wapi tunapomuona Yesu au Mitume wakizungumzia mafanikio kwa mtazamo wa jinsi hii? Jambo lililo wazi ni kwamba Mungu ameahidi kuyashughulikia maisha yetu (Mathayo 6:25-26); ni udhihirisho wa moyo wa Mungu kwa watu wake na maono yake kwa ajili ya Ufalme. Biblia sio kitabu chenye mbinu na kanuni kwa wahubiri kutumia ili kuwaomba ninyi muwape pesa ili Mungu aweze kuwabariki. 25

Kumpenda Yesu, Kuupenda Ufalme Wake Mpango wa Mungu kwa Kanisa lake ni kwamba Wakristo wabebe moyo wake uwe ushuhuda kwa ulimwengu usioamini. Kwa Mkristo mwenye shukrani anayejua kuwa Yesu alitoa kila kitu kwa ajili yake, ambaye moyo wake unamilikiwa na Mungu na ambaye maisha yake yamebadilishwa na Kristo, kutamani kumtolea Mungu ni asili yake. Si mtu anayeleta matoleo yake kwa sababu analazimika kufanya hivyo, au kwa sababu mtu fulani amemwambia atoe kiasi fulani, au kwa kuwa amefundishwa jinsi ya kumtolea Mungu. Na hakika hatoi ili abarikiwe. Anatoa kwa sababu anampenda Yesu na Ufalme wa Mungu; ana shukrani kwa ajili ya wokovu. Maisha yake yamefananishwa kikamilifu na ya Kristo, na moyo wake umetolewa kikamilifu katika kuyatumikia maono ya Mungu kwa Kanisa lake. Hapa yupo mtu mwenye uwezo wa kutoa vyote, juu sana kuliko asilimia yoyote iliyopangwa au kiwango chochote kilichowekwa. Yeye hupanda kwa furaha katika Ufalme wa Mungu kwa kadiri anavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Mkristo wa aina hii anaweza kutoa kwa ukarimu hata katika nyakati za uhitaji mkubwa, kama tunavyoona Kanisa la Makedonia likifanya katika 2 Wakorintho 8. Anatenda huku akiamini ya kuwa Mungu atashughulikia mahitaji yake binafsi, kwa sababu anajua moyo wake ni kwa ajili ya Ufalme. 26

Sura ya III - Mkristo na Pesa Mungu Anataka Tufanikiwe Kuna vifungu viwili vya Maandiko ambavyo karibu kila Mkristo anavijua; kwani, katika nyakati fulani, wengi wetu huenda tumesikia vikifundishwa kuhusiana na utoaji na mafanikio. Katika maeneo yote mawili, mafundisho ya uongo yamepenyezwa Kanisani ikiwa ni matokeo ya wahubiri kuichukua mistari hii kwa maana nyingine Katika 3 Yohana 1-8 tunasoma, Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. Sote tunafahamu kuwa Mtume Yohana anamsifu Gayo kwa moyo, upendo, jinsi anavyoujali Ufalme, na ukarimu wake kwa watu wa Mungu. Je, si ni jambo la kawaida kabisa kwa Yohana kumtaka Mungu ambariki mtu wa jinsi hii? Mtume anataka Gayo afanikiwe katika mambo yake yote, kwa sababu anajua chochote anachopewa na Bwana kitatumika kuwabariki ndugu wengine na kitakuwa na manufaa katika Ufalme. Sasa, tunarukaje kutoka kwenye kweli hii hadi kutangaza kuwa ni mapenzi ya Mungu - ni kusudi lake na mpango wake - kwamba Wakristo wote wafanikiwe kifedha; kwamba Wakristo wote wanapaswa watarajie kupokea mara mia kama malipo, endapo watatoa kwa ajili ya mhubiri huyu au mradi ule? Hili ni kinyume na Maandiko! Tunachoweza kusema bila shaka yo yote ni kwamba Mungu angependa kumbariki kila Mkristo, ambaye, kama Gayo, ana moyo kwa ajili ya Ufalme, na ni mkarimu kwa watu wa Mungu. 27

Maono Ya Agano Jipya Tunaposoma maneno ya Yesu katika Luka 6, tunaona roho ile ile na moyo ule ule aliokuwa nao Yohana na mitume wengine wote. Hapa (mistari 27-46) Yesu anazungumza na makutano kuhusu kuwa na moyo mwingine na maono mengine... moyo na maono ya Ufalme. Anawasihi watu kutoa maisha yao na kumruhusu Mungu awabadilishe ili waishi sawasawa na Agano Jipya. Kwamba, katika mtazamo huu anasema katika msitari wa 38: Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, si sababu ya mtu kutafsiri kuwa alikuwa akizungumzia utoaji na mafanikio. Hiki kifungu kinahusu aina ya moyo anaopaswa kuwa nao Mkristo ambaye daima anashughulishwa na Ufalme wa Mungu. Kwa msingi huo Yesu anamalizia, katika msitari wa 46 kwa kusema, Na kwa nini mnaniita Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? Kwa hiyo, hapaswi mtu yeyote kutumia andiko hilo kushawishi watu ya kuwa wakitoa, bila kujali hali za mioyo yao au nia wanayotoa nayo, ya kwamba Mungu bado anawajibika kuwabariki. Hii ndiyo maana leo hii kuna mamilioni ya Wakristo ambao bado wanasubiri baraka zao! 28

Sura ya III - Mkristo na Pesa Kwa Kadri Ya Uhuru Wa Moyo Wako Niruhusu niseme ya kwamba ikiwa bado unaamini kuwa unalazimika kumtolea Mungu, hujaelewa undani wa kile ambacho Yesu Kristo alifanya pale msalabani; ukombozi aliotupatia Mwana wa Mungu. Ametuweka huru. Leo hii tuko huru kutoa kutoka katika ndani ya mioyo yetu, kwa kadiri tunavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Je, unafahamu ya kuwa kama nitamtegemea mtu au sheria yoyote katika Agano la Kale iliyo chini ya ukuhani wa ki-lawi kuniambia ni kiasi gani ninachotakiwa kutoa, ninaweza nikajikuta nikitoa chini zaidi ya kiwango nilichodhamiria moyoni kutoa? Sasa katika mtazamo halisi tunaona moyo wa Mkristo wa Agano Jipya katika tamko la Mtume Paulo katika 2 Wakorintho 9:7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Hapa hatuoni Mkristo mwenye hofu, na mnyimivu, anayelazimika kutoa kwa sababu anawajibika kutoa, au kwa sababu kila mtu atafahamu kiasi alichotoa. Kutumika Katika Uhuru Makanisa ya Makedonia yalikuwa na uwezo wa kutoa licha ya umaskini wao mkubwa, ikiwa ni matokeo ya Injili iliyowafanya kukubali 29

kupoteza maisha yao, kujikana nafsi zao, kuuchukua msalaba kila siku na kumfuata Yesu. Ukarimu wao ulikuwa ni matunda ya kazi ya injili, si matokeo ya kulaghaiwa kihisia. Walitamani kutoa kutoka katika vina vya mioyo yao, na wakasisitiza kutaka kushiriki katika mradi wa kiroho na wenye manufaa kwa Ufalme na kwa watakatifu wengine. Tafadhali elewa kuwa sitaki kukufanya uangalie nyuma na uanze kuhoji ni kwa jinsi gani au ni kwa lipi ulilotolea pesa zako huko nyuma. Lakini ninaamini kuna Wakristo wengi wanaotafuta kuujua ukweli. Nami ninachotaka ni kwa Kanisa kuujua moyo wa Mungu kwenye suala la pesa; fundisho la kweli ni lipi kulingana na Neno lake ili, kwa neema yake na kwa kuongozwa na Roho wake Mtakatifu, tuweze kuwa huru kumtumikia Mungu kwa pesa zetu. 30

Sura ya IV Mungu na Muziki 31

Sitakuwa ninatia chumvi nikisema ya kwamba uzi unaotenganisha muziki wa kidunia na kile kinachoitwa Muziki wa Kikristo wa Kizazi Kipya, ni mwembamba kwelikweli. Inasikitisha, lakini uimbaji mwingi tunaousikia Kanisani siku hizi ni muziki wa kidunia wenye maneno ya Kikristo. Kwa kadiri roho wa dunia hii inavyozidi kujipenyeza Kanisani, si ajabu kuuona muziki wake pia ukiingia Kanisani. Tunapotazama muziki na uimbaji wa Kikristo ulioko sasa hivi, tunapata kuona ni kwa kiasi gani roho ya ulimwengu ilivyolivamia Kanisa. Kwa kadiri uimbaji Kanisani unavyozidi kuchukua sura ya kidunia tunaona jinsi hili linavyoleta kuchanganyikiwa na kumenyana, hasa kwa vijana. Swali ninalotaka kuuliza ni: Je, kuabudu halisi kuna uhusiano gani na muziki wa kidunia? Ninashindwa kuelewa ni kwa nini tutake na hata tujaribu kuyachanganya, haya mawili kumsifu Bwana kwa mdundo wa kidunia kwa kweli, haiwezekani! Tunapokuwa tumezaliwa mara ya pili, tunapaswa tutamani kuabudu kwa mioyo yetu, katika Roho na Kweli. Jambo lolote nje ya hilo ni kuuburudisha mwili. Kwa mara nyingine tena, ninaamini ya kwamba katika kuliangalia Neno la Mungu tutapata ufahamu na ufunuo mpya juu ya moyo wa Mungu katika suala la sifa na kuabudu. Hebu tuwe makini tusikaribishe kila kitu kinachobeba nembo Kristo ya kwamba kinampatia Mungu utukufu. Hakuna maelekezo ya wazi katika Biblia kuhusu namna tunavyopaswa kumuabudu Mungu. Katika Agano la Kale kuna maagizo 32

Sura ya IV - Mungu na Muziki yanayohusiana na muziki, kuabudu, na vyombo vya muziki, pamoja na mifano ya watu wa Mungu wakimsifu Mungu kwa shangwe na kucheza; lakini katika Kanisa la Agano Jipya hakuna maelekezo juu ya aina ya maneno, mapigo, au midundo tunayoweza kutumia; au hata namna ya kucheza. Kuna sababu nzuri juu ya hili... kumbuka kuwa sisi ni watu wa Agano Jipya! Kwamba ni weusi au weupe, tajiri au maskini, wasomi au wasio wasomi, sote tuna vitu viwili vinavyofanana: mioyo yetu na Roho Mtakatifu aliyeko ndani yetu. Yeye ni mwalimu wetu, anatuongoza na kutushuhudia mioyoni mwetu juu ya nini kinachotokana na Mungu Baba na nini kisichokuwa cha Mungu. Roho Mtakatifu Ni Mwangalizi Wetu Katika Yohana 16:13-14, tunasoma, Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Hakuna kuchanganya hapa: Ni wazi kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuelekeza, kutufundisha na kutuongoza katika namna Yesu anavyonena na namna anavyotenda. Sote tutakubaliana kuwa kulikuwa na harufu nzuri ya manukato katika yote Yesu aliyosema na kufanya. Vivyo hivyo, harufu ya manukato ya kumjua Kristo inapaswa iambatane na yote tunayosema na kufanya. Cho chote kinachotokana 33

na dunia kina roho nyingine; lakini kwa sababu Mungu ametupa sisi (Wakristo tuliozaliwa mara ya pili) Roho Mtakatifu kuishi ndani ya mioyo yetu, tunaweza kupambanua roho ya ulimwengu huu ulioko chini ya milki ya Shetani. Mambo Ya Ajabu Yanafanyika Ninaamini watu wanaelewa ya kuwa hata katika Ukristo kuna mambo ya misisimko na ya kimwili yanayoendelea. Kwa bahati mbaya si kila kitu chenye nembo ya Ukristo ni kizuri kwa moyo wako au roho yako. Kama ilivyo kwamba kuna aina ya uimbaji na muziki ambavyo tunashuhudiwa mioyoni mwetu ya kuwa vinatokana na Bwana, vivyo hivyo kuna aina ya muziki, uimbaji na kucheza ambavyo vinatoa harufu kali ya kidunia na ya mwili. Tuwe makini tusibebe Neno la Mungu katika hali ya maandiko tu. Neno linaposema Msifuni Bwana kwa vinanda au Msifuni kwa kucheza na shangwe, haina maana kwamba tunaweza kuleta roho ya dunia Kanisani, kwa kucheza kwa namna yoyote tunayojisikia, au kwa kutumia vyombo kucheza midundo au mitindo ambayo huwezi kutofautisha na ile inayochezwa katika kumbi za muziki. Kwa kuangalia mifano michache tu ya kucheza na kushangilia katika Biblia, ninaamini tunaweza kuona tofauti kati ya muziki na kuabudu kunakompendeza Mungu kwa kuashiria kile kilichomo ndani ya 34

Sura ya IV - Mungu na Muziki mioyo yetu, na muziki unaotumbuiza tu na kulisha miili yetu, ambao mwisho wake ni kutupeleka katika kutenda dhambi. Katika Kitabu cha 2 Samweli 6:12-15, kuhusiana na wakati ambapo Daudi aliporejesha sanduku la agano, lililowakilisha uwepo wa Mungu katika Yerusalemu, mistari ya 14-15 inaeleza, Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la BWANA kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta. Daudi pamoja na watu wa Israeli walikuwa wanasherehekea ushindi mkubwa. Kicho chake kwa Mungu, unyenyekevu wake, pamoja na furaha ya kweli vilizidi sana ndani yake kiasi cha kumfanya acheze, licha ya kuwa tendo lile lilionekana kama la kipuuzi mbele ya mke wake. Watu walifurahia kile ambacho Mungu alikuwa amefanya, walijua hii haikuwa kazi ya mwanadamu. Daudi alipomuua Goliathi, watu wale wale waliokuwa wakitetemeka kwa hofu ghafla walijawa ujasiri wakatoka kwenda kuwashambulia Wafilisti. Baada ya kuwa wametoka kwenye vita kama hiyo, tunasoma katika 1 Samweli 18:6-7 kwamba, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki Mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. Nao wanawake wakaitikiana wakicheza. Katika Agano Jipya (Matendo ya Mitume 3) Petro na Yohana walienda hekaluni siku moja, na mtu mmoja aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa akaponywa. Mtu huyu alishangilia kwa furaha kuu na kucheza ndani ya hekalu akimsifu Mungu kwa muujiza wake. Hakuweza kujizuia katika furaha yake. 35

Shangwe Itokayo Moyoni Katika mifano yote mitatu, tunaona mlipuko wa shukrani na shangwe, vilivyotokana na moyo wa shukrani uliosababisha kuimba, kucheza na muziki. Ni suala la Mungu, wala si muziki. Tunaponyenyekezwa na kile ambacho Mungu ametufanyia, tuko huru kufurahia kwa kadiri mioyo yetu itakavyotuongoza. Hakuna tatizo juu ya kuimba na kucheza katika mazingira kama hayo. Lakini viongozi wa sifa wanapoamua Jumapili asubuhi kwamba sasa ni wakati wa kuanza kumsifu Bwana kwa kucheza, au kuabudu kwa kushawishi hisia za watu, kwa uimbaji ambao si kingine bali ni maneno ya Kikristo yaliyoambatana na midundo ya kidunia na yanayotupelekea katika kuigiza, ni lazima tuanze kujiuliza maswali. Na ni vivyo hivyo kwa Matamasha ya Injili. Je, ni nini kinachotokea kwa hawa vijana wa kike na wa kiume ambao hisia zao na miili yao inakuwa imeamshwa kwa hali ya juu na waimbaji walioko jukwaani? Yesu anapewaje heshima na utukufu katika mazingira haya? Wengine wanaweza kusema hiyo ndiyo namna vijana wa kisasa wanavyoabudu na ni njia ya kuwavuta marafiki zao kuja kusikiliza habari za Bwana Yesu. Lakini mimi naweza kuuliza je! ni wangapi katika hawa marafiki wanaofikia kwenye kuzaliwa mara ya pili kwenye haya matamasha? Na, cha muhimu zaidi, je! ni idadi gani ya hawa Wakristo vijana wanaojikuta sasa wakiwa katika barabara ya kurudi nyuma kiroho ikiwa ni matokeo ya kuwasha tamaa 36

Sura ya IV - Mungu na Muziki za miili yao kupitia haya matamasha? Mimi binafsi ninapoyasikiliza au kuyatazama matamasha kama haya, Roho Mtakatifu hushuhudia ndani yangu kuwa kuna kitu hakiko sawa. Na sote tunajua ni nani na ni nini kilichoko nyuma ya kila kitu ambacho hakitokani na Roho! Hatuwezi kujificha nyuma ya muziki wa injili unaofurahisha hisia zetu na kuamsha miili yetu. Mwili hauwezi kutoa uzima wa rohoni, kwa hiyo, mara tu mwili unaposisimkia aina fulani ya muziki tuko hatarini. Sisi kama watu wa rohoni ni lazima tuweze kupambanua kati ya muziki utokanao na Mungu - ibada ya moyoni inayojenga - na muziki wa kidunia unaoamsha tu miili na hisia zetu. Muziki Una Vyanzo Viwili Kama tunavyojua, muziki unatokana na mmojawapo ya vyanzo viwili tu. Chanzo cha kwanza ni katika moyo wa Mungu - ambapo wanaume na wanawake, mara nyingi kutokana na kazi ya Mungu waliyoishuhudia maishani mwao, huongozwa na Roho Mtakatifu kutunga sauti au kuandika wimbo. Nyingi za tenzi kuu za Kikristo tulizonazo leo hii zinalishuhudia hili. Mungu ndiye anayeumba huu muziki moyoni mwa mwanadamu ili amwabudu na kumsifu Yeye, kumpa utukufu wote, heshima na uweza. Upako wa Mungu unapokuwepo, mioyo yetu inayeyuka na tunamezwa katika uwepo wake. Chanzo cha pili cha muziki ni roho inayoutawala ulimwengu - ambapo midundo, vionjo na miondoko ni ya kimwili na ya kidunia. 37

Muziki ni eneo lingine la hatari sana kwa Kanisa tunapouweka kando msingi, yaani, Injili ya Msalaba, ambayo mara zote inatupa changamoto na kutuleta kwenye utu uzima. Tukikaa kwenye huo msingi, kwa kadiri tunavyozidi kukua na kufanana zaidi na Kristo, tutafahamu pasipo na shaka yo yote ni lipi tufanye, wapi pa kwenda, na kipi cha kusikiliza. Na tutajikuta hatuvutiwi tena na muziki ambao hauifaidi roho kwa namna yoyote. Ninataraji ya kuwa maneno haya machache yameleta mwanga na ufafanuzi zaidi kuhusiana na somo hili; ya kwamba kwa namna fulani Mungu ameyafungua macho yako na umetiwa moyo 38

Sura ya V Vita ya Rohoni 39

Fundisho lingine ambalo limejipenyeza Kanisani ni lile la vita vya kiroho. Wakristo kila mahali wanatilia mkazo katika kutoa pepo na kudhibiti roho chafu kila mahali wanakokwenda. Ikiwa tunataka kuishi sawasawa na fundisho la uzima la Kristo, tunapaswa tuyachunguze Maandiko tuone ni nini kilichomo moyoni mwa Mungu, na katika mioyo ya Mitume walioandika Nyaraka. Leo hii katika mengi ya makanisa, kuna lugha nyingi na shughuli nyingi linapokuja suala la vita ya rohoni, na kifungu cha Biblia kinachotumika katika hili suala ni Waefeso 6. Hata hivyo, ninapokitazama hiki kifungu, sioni jambo lolote linazungumzia kuanzisha mapambano dhidi ya roho wachafu. Ninachoona ni wito halisi wa Mungu juu ya maisha ya muumini. Mtume Paulo anatuhimiza tujitie nguvu katika Bwana, ili tuweze kusimama siku ya uovu. Mahali pengine, Mtume Yakobo anatuagiza ya kwamba adui ashambuliapo: Mpingeni Shetani naye atawakimbia. Sehemu kubwa ya kile Kanisa linachokiita vita vya kiroho si kingine zaidi ya kupigana na mapepo. Wakristo wanaona hiyo kuwa ndiyo njia ya kupata ushindi maishani mwao. Lakini, Biblia inasema waziwazi ya kuwa ikiwa tuko ndani ya Kristo, Shetani hawezi kutugusa. Ikiwa maisha yetu yako sawa mbele za Mungu, na mioyo yetu ni safi, ni kwa nini tuyaogope mapepo? Tunapaswa tu kuyapinga. Tumeitwa tuishi maisha yenye ushindi, na tutaupata huo ushindi na kupinga mashambulizi ya Shetani tutakapoyafuata maagizo ya Yesu katika Mathayo 16:24: Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. 40

Sura ya V - Vita ya Rohoni Tunapoyaangalia Maandiko katika mtazamo sahihi, na kupata ufahamu sahihi wa kile kilichofanyika Msalabani, tutaanza kuona nafasi yetu na msimamo wetu katika Kristo na katika Neno lake. Ninaamini wale wanaojishughulisha na vita vya kiroho wanapaswa wajiulize maswali matatu Vita vya kiroho ni nini hasa? Hili limetajwa wapi kwenye Agano Jipya? Na, Je, dhabihu ya Yesu Msalabani haikutosha? Katika Waefeso 6, ninaamini Mtume Paulo anazungumzia maisha ya ushindi pamoja na Bwana, maisha yenye ushindi katika haki na maisha matakatifu yanayompendeza Mungu. Kwa namna fulani, hii mistari imetafsiriwa kwa namna isiyo sahihi kuleta maana ya kwamba vita ya rohoni ni sehemu ya wito wetu. Leo hii, Kanisani kumeingia uelewa fulani ya kwamba, ikiwa tunataka ushindi, tunahitajika muda wote kuwa vitani tukipigana na mapepo, roho chafu, na kila nguvu na mamlaka; kufunga na kufungua roho kila tupatapo nafasi kwa sababu wametuzunguka kila mahali. Hebu tuangalie mistari ya 10-11: Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, n.k... Kusudi la hili andiko sio kutufundisha jinsi ya kupigana vita ya rohoni. Wito uliopo hapa ni kwamba tuimarike, kwa sababu adui atashambulia! Paulo anasema, Muimarike katika Kristo kwa sababu siku ya uovu imewadia. Mtume anaelewa fika ya kuwa vita au mapambano yo yote maishani mwetu hakika ni ya rohoni, na 41

wala si kitu cha kimwili au cha asili. Anatuonya mapema ya kwamba tunapaswa kuwa hodari katika Bwana. Kwa maana nyingine, ikiwa tu imara rohoni hatutashindwa na hila za adui. Ufunguo wa hili ni shauku yetu ya kutaka kukua, na utayari wa kuyasalimisha maisha yetu kikamilifu kwa Kristo. Hapo Bwana atatupa neema ya kusimama, hata kama tu wachanga kiroho, tunapozidi kumpinga Shetani. Mungu hatamruhusu adui avuke mpaka kwani yeye ndiye mlinzi wetu; yeye ni ngao na mwokozi wetu. Shauku kuu ya Paulo ni kwamba tumtumikie Bwana katika hali zote na ya kwamba adui ashambuliapo, tuwe hodari katika imani ili tuweze kusimama imara na kuupata ushindi. Kumtii Mungu Mtume Yakobo anasema katika waraka wake (4:7-8): Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi... Roho iliyoko nyuma ya mistari hii ni sawa na ile iliyo kwenye Waefeso 6; mwito ule ule, maisha yale yale, mamlaka ile ile! Anaposema tuyatiishe maisha yetu kwa Mungu, anamaanisha kujikana nafsi zetu, kuuchukua msalaba wetu, na hatimaye, kumpinga Shetani. 42

Sura ya V - Vita ya Rohoni Tutawezaje kubaki mwilini halafu tuende vitani dhidi ya mapepo, na falme, na kudai na kufundisha ya kuwa tutapata ushindi dhidi yao? Huku ni kuyatumia Maandiko kama mbinu, na inakwepa ukweli ya kwamba Ukristo ni maisha tunayoishi katika roho. Silaha Zote Za Mungu Ni vigumu kumshinda Shetani ikiwa hautembei kwenye barabara ya Msalaba na kumruhusu Mungu akutakase na ashughulike na mwili wako. Unaweza ukanukuu kila Andiko, ukafunga kila pepo, ukakiri kila msitari, ukachukua mamlaka dhidi ya kila jambo, na kufunga na kufungua kwa kadiri upendavyo. Ikiwa maisha yako ya rohoni yamevurugika, na hayako juu ya msingi wa Kristo aliyesulubiwa, adui hatakimbia utakapojaribu kumpinga; badala yake, atakuingiza dhambini na kukushinda. Jumbe nyingi zimehubiriwa, na vitabu vimeandikwa, juu ya kuvaa silaha zote za Mungu. Hakika hii haiwezekani iwe ni kanuni ya kimwili; wala haihusikani na kuyanukuu Maandiko, kufunga mapepo, n.k. Si suala la maneno hata kidogo. Silaha yetu ya rohoni inapatikana katika hali za mioyo yetu, maisha yetu matakatifu, na roho wa maombi. Mamlaka yetu inapatikana katika utakatifu wa maisha yetu ya rohoni. Ushindi unapatikana kwenye barabara ya Msalaba! 43

Kwa hivyo, je! kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake inamaanisha nini hasa kwa maisha yetu ya siku kwa siku? Tukiunganisha yale wanayoyasema Paulo na Yakobo, ni kwamba ni wakati tunapoyaweka maisha yetu katika mkono hodari wa Bwana. Ni wakati tunapoifungua mioyo yetu kwa ajili ya kuupokea ufunuo wa injili na kumruhusu Mungu kutenda kazi ndani yetu, inayotupeleka kwenye maisha ya imani, haki, maombi, n.k. kwa maana nyingine, tunazivaa silaha zote za Mungu. Kwa jinsi hiyo tunaupata ushindi bila kumenyana na mapepo mchana kutwa. Na, Shetani anapokuja, tunahitajika tu kumpinga bila kufanya jambo lingine zaidi. Huo ndio wito, ndugu na dada zangu. Si kuingia kwenye mapambano ya kiroho dhidi ya mapepo Maisha yetu yanapokuwa juu ya msingi sahihi, tunakuwa na mamlaka ya Mungu katika kumpinga Shetani. Kila anaposhambulia na sisi kumpinga, Shetani hana budi kukimbia. Sote tunakubali ya kuwa mapepo na roho chafu wapo, ila Yesu Kristo amewashinda wote (Wakolosai 2:15). Ndio maana, maisha yetu yanapokuwa yametiishwa kwa Mungu, hatutaogopa mapepo, wala kuyatafuta kila mahali. Mamlaka Ya Mungu Hebu sasa tuangalie Mathayo 16:18-19. Yesu anasema, Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga 44

Sura ya V - Vita ya Rohoni kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Bwana wetu alimpa Petro mamlaka kuliongoza Kanisa lake. Anamwambia, Lo lote utakaloamua na kutamka duniani kulingana na mpango wangu na mapenzi yangu, kwa manufaa ya Ufalme, nitakutetea nikiwa mbinguni na nitalifanikisha. Mfano wa hii mamlaka ikitenda kazi unaonekana katika Matendo 5. Akiwa mtu wa imani na maombi, aliyeishi maisha matakatifu na ya haki, Petro alivaa silaha za Mungu, na akaongozwa na Roho Mtakatifu kunena sawasawa na mapenzi ya Mungu. Akafahamu kile Anania na Safira walichokuwa wamekifanya, na akanena kwa mamlaka ya Mungu. Alichofunga duniani kikafungwa na mbinguni. Ninamwona Petro akitekeleza jukumu lake la uongozi, pamoja na mamlaka aliyopewa na Bwana. Kumpinga Shetani Mara nyingine tunahitajika kumpinga Shetani, na kumzuia na kumsimamisha katika kazi zake. Lakini hii haiwezi kuwa mbinu tutakayotumia katika maisha yetu ya siku kwa siku. Paulo na Sila walipowekwa gerezani, hawakuanzisha kipindi cha vita ya rohoni; Biblia inasema walianza kumtukuza Mungu. 45

Hawakuhitaji kufunga mapepo au roho yo yote ili wafunguliwe. Mioyo yao ilikuwa sawa, maisha yao yalikuwa kwenye utaratibu wa roho na walimwabudu Mungu, huku wakifahamu ya kuwa ukombozi wao ulikuwa karibu. Muda si mrefu, Mungu akalitikisa gereza na kuwaokoa. Paulo alipofika Athene, Biblia inasema alichukizwa na sanamu na miungu waliyoiabudu. Je, Mtume alianza kufunga mapepo? Hapana! Alinena waziwazi, akiwaambia ya kuwa waliabudu kila aina ya miungu, ila yeye angewaambia habari za Yule waliyepaswa kumwabudu. Akanena habari za Mungu wake, na akawahubiria habari za Yesu Kristo. Tunaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, tunaona wanafunzi walitumia muda wao wakiihubiri Injili. Walipokutana na mazingira ya kuhitaji kumpinga adui, walifanya hivyo na kuendelea na kazi ya huduma. Hebu tusitekwe akili na kutumia muda mwingi tukishughulika na mapepo, badala ya kuiishi na kuishiriki Injili, na kumtumikia Kristo kwa mioyo yetu yote. 46

Sura ya VI Mahusiano Kabla ya Ndoa 47

Kama kuna eneo Kanisani leo ambapo kuna mkanganyiko mwingi, na ambapo kuna ushahidi ya kwamba mfumo wa ulimwengu umejipenyeza tena na kuathiri namna Wakristo wanavyofikiri na kuenenda, ni katika mahusiano kabla ya ndoa. Ingawa hili somo linaweza kuonekana kama linawahusu tu vijana wanaotaraji kufunga ndoa, ukweli ni kwamba ni jambo linalohusika na Wakristo wote. Katika hili suala, Kanisa linaonekana kuamua kuchukua mitazamo miwili inayokinzana kabisa. Leo hii tunaona ama sheria au uhuru usiokuwa na mipaka. Katika baadhi ya makanisa kuna sheria kuhusu kile watu wanachoruhusiwa kufanya au kutokufanya, ilhali katika mengine, hilo suala halizungumziwi kabisa. Hakuna mmojawapo ya hii misimamo ulio sahihi! Ninaamini kwa dhati ya kwamba Kanisa limeutelekeza wajibu wake kwa kutokuchukua msimamo wa wazi wa Kibiblia kuhusu namna Wakristo, na hasa vijana, wanavyopaswa kuishi maisha halisi ya Ukristo, iwe ni kabla ya au baada ya kufunga ndoa. Katika kukaa kimya na kuruhusu viwango na fikra za kidunia kuingia Kanisani, tumeacha kuisimamia Kweli ya Injili, na tumejichanganya. Matokeo yake ni kwamba Wakristo wanajiingiza kwenye mahusiano yasiyokuwa ya rohoni na ambayo hayawasaidii kukua na kumtumikia Bwana katika njia sahihi na mara nyingi yakiwapelekea katika kutenda dhambi na kuwaondoa mbali na mpango wa Mungu kwa maisha yao. 48

Sura ya VI - Mahusiano Kabla ya Ndoa Kwa ujuzi nilionao ninafahamu ya kwamba Injili inapoyakamata maisha ya vijana, hawamenyani, au kuhisi kusukumwa au kuchanganyikiwa juu ya kile kinachoruhusiwa katika mahusiano yao, au ni wapi wanapaswa kuchora msitari. Kinyume chake, hawahitaji sheria za kuwaambia ni lipi wafanye na lipi wasifanye. Wanafahamu waziwazi mpango wa Mungu ni upi juu ya maisha yao na wanatamani kutenda mapenzi ya Mungu, kubaki wasafi, na kuenenda katika njia inayompendeza Mungu. Tunapoliangalia Neno la Mungu katika mtazamo wake, ninashawishiwa kufikiri ya kwamba dhana zetu kuhusu kuchumbiana, kuwa na marafiki wa kike na marafiki wa kiume, na mahusiano kwa ujumla zitabadilika! Ulimwenguni, mahusiano ya karibu ya kimwili kabla na nje ya ndoa yanakubalika, na hata kushabikiwa. Vipindi vya uchumba vinahesabika kama nyakati za wahusika hao wawili kuona kama wanafaana. Hili mara nyingi linawapelekea katika kuwa na mahusiano ya kimwili kabla ya ndoa. Inasikitisha kwamba katika makanisa mengi vijana wanauiga mtindo huu huu, na wale walio katika nafasi za mamlaka viongozi wa kanisa, wazazi, n.k., hawashughuliki na hili suala kwa umakini unaohitajika. Vijana wanaachiwa kujiamulia wenyewe mipaka katika hili suala nyeti, badala ya kupewa miongozo ya Kibiblia iliyo wazi. Hebu tuwe wazi tokea mwanzo ya kwamba Mungu hachanganyikani; Neno lake halijaficha jambo. Ndani mwake, tunaona maono na 49

mpango wake ulio dhahiri, kwa watu wake na kwa Kanisa lake. Ni wazi kwamba hataki tujichanganye na ulimwengu na njia zake. Na wala Mungu hataki sheria na kuhukumiana Kanisani mwake, ambavyo havina nguvu yoyote ya kumbadilisha mtu. Anachotaka ni Wakristo wote wahakikishiwe na Roho Mtakatifu kuhusu dhambi kupitia Injili ya Yesu Kristo ambayo inaweka mpaka ulio wazi na kutuonyesha tunapaswa tusimame juu ya msingi upi. Hii ndiyo maana ninaamini tunapaswa kurejea kwenye msingi Neno la Mungu ili tuone Mungu anasemaje juu ya hili suala. Miili Yetu Ni Viungo Vya Kristo Hebu tuangalie Mungu anavyoiona ndoa na mahusiano nje ya ndoa, na tutafahamu ya kwamba uhusiano wowote wa kimwili nje ya ndoa, uwe wa aina yo yote ile, unahesabika kuwa ni dhambi machoni pa Mungu. Si suala la Tuweke wapi mipaka? kwa sababu tukijaribu kuweka mipaka ya aina yoyote, tutaivuka tu. Ni kama lile tangazo la breki za magari lisemalo, Usianzishe jambo ambalo hutaweza kulizuilia! 1 Wakorintho 6:15 inasema: Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Kwa hivyo, si roho zetu tu zilizounganika na Kristo; nafsi yetu yote ni moja naye. Mistari ya 16 17 inasema, Au hamjui 50

Sura ya VI - Mahusiano Kabla ya Ndoa ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. Paulo hapa anasema waziwazi ya kwamba ni lile tendo la ndoa linalowaunga watu wawili kuwa mwili mmoja, na hili linapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Katu hatupaswi kusahau ya kuwa roho zetu, nafsi zetu na miili yetu imeungwa pamoja na Kristo. Siku hizi Wakristo wengi wanafanya wanavyopenda na miili yao, pasipo kutambua madhara ya rohoni yanayotokana na matendo yao. Kwenye kifungu hiki Paulo anaweka utofauti kati ya dhambi ya mwili na dhambi nyingine; katika zinaa unatenda dhambi dhidi ya mwili wako kwa sababu unafanyika kuwa mmoja na yule mnayeunganika naye kimwili. Uzinzi ni uhusiano wowote wa kimwili nje ya ndoa. Uongo, wizi, hasira, n.k., ni tofauti; haya ni matunda ya tamaa zetu za kimwili. Ikiwa Mungu aliamua kuweka utofauti kati ya dhambi ya mwili na dhambi nyingine, tunapaswa kuwa makini sana, na kuufahamu moyo wake katika hili suala. Msitari wa 18 unasema, Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Hatupaswi kusahau ya kuwa miili yetu pamoja na roho zetu vimeungwa na Kristo, na tunapotenda zinaa ni jambo zito sana machoni pa Mungu. Mistari ya 19-20 inatukumbusha ya kuwa mwili wetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na tunahimizwa, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. 51